Afisa Mazingira wa Airtel Bwana,
Ncheye Mazoya na Katibu tarafa wa Kinondoni Bw, Fortunatus Fulgence
Isakafu wakikabidhi mapipa yakukusanyia uchafu kwaajili ya mtaa wa kumbukumbu
kwa Diwani wa Kata ya Kinondoni Bw, Mustafa Muro na Mwenyekiti wa Mtaa
Kumbukumbu Bw, Shaban Majeshi. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika
ofisi ya serikali za mtaa huo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imetoa msaada wa mapipa 15 ya kukusanya na kutunzia takataka
kwa serikali ya mtaa wa kumbukumbu kata ya kinondoni yenye thamani
shilingi milioni 3 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika
shughuli mbalimbali za kutunza mazingira ili kuiwezesha jamii kuishi katika
mazingira bora yatakayopelekea kuwa na afya bora.
Akiongea wakati wa hafla ya
makabidhiano Afisa mazingira wa Airtel Bwana, Ncheye Mazoya alisema “Airtel
tunatambua sana jitihada zinazofanywa na serikali ya Jamuhuri ya muungano wa
Tanzania katika kutunza na kuweka mazingira ya jamii kuwa safi. kwetu
sisi Airtel Tunaamini kwamba ili tuweze kufanya biashara lazima
tuwe na mazingira safi na wateja wenye afya bora, na ndio maana leo hii
tunaunga mkono harakati za serikali za kuhakikisha swala hili la kufanya usafi
kila mahali linaendelea kufanikiwa
“Tunaamini mapipa haya ya
kutunzia taka yatasaidia jamii inayotuzunguka hapa kinondoni na kuweka
mazingira katika hali ya usafi na kusaidia kuepusha magonjwa ya milipuko ambayo
yamekuwa ni changamoto kubwa sana nchini” alieleza Mazoya
Kwa upande wake Katibu tarafa wa
Kinondoni Bwn Fortunatus Fulgence Isakafu Aliwapongeza Airtel kwa mchango wao
na kuongeza kwamba tarafa yake ina mpango mkakati wa kutekeleza kwa
vitendo kampeni ya usafi kwa kuhamasisha jamii kujitolea katika kutunza mazingira
yanayowazunguka na kuyaweka kuwa safi wakati wote.
“Airtel msaada wenu umekuja wakati
sahihi kwa kuwa zoezi la usafi kwetu sisi ni endelevu, mapipa haya ya kuhifadhi
taka yatasaidia sana kupunguza kuzagaa kwa taka kila mahali na
kurahisisha ukusanyaji taka kwa ajili ya kuzipeleka sehemu maalum kwa
uteketezaji”
Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali
kutuunga mkono na kuungana nasi katika kampeni hii kama walivyofanya wenzetu wa
Airtel leo. Alimaliza kwa kusema Bwn, Isakafu
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Airtel donates cleaning equipment
to Kumbukumbu ward
Airtel Tanzania has donated 15
dustbins worth three million shillings to kumbukumbu ward in kinondoni
municipal in facilitating easy waste management and commits to collaborate with
government in environment conservation initiatives
Speaking during handover
Airtel environmental Officer Ncheye Mazoya said” Airtel recognized government’s
effort in keeping environment clean and safe, in this line we have
decided to join hands with government to support community by providing
essential waste keeping tools for easy collection and management of wastes.
“We believe the aid will promote
health environments and help in preventing epidemic diseases which has been a
major challenge in the country”. Added Mazoya
On his side, Magomeni Division
Administrative Secretary, Fulgence Isakafu applauded Airtel for their valued
contribution and further said kinondoni ward has lot of initiative including
involving the community to willingly participate in keeping the environment
clean at all times.
“The general cleaning campaign is
ongoing exercise; we thank Airtel for providing us with dustbins for ease waste
collection and keeping. We call for other stakeholders to support this
initiative. Added Isakafu
No comments:
Post a Comment