Tangazo

July 12, 2016

DC BUHIGWE ATOA SIKU SABA KUKAMILISHA MFUMO WA NYUMBA KUMI ZA KIUSALAMA



Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti.
*******
MKUU Wa Wilaya ya Buhigwe, Mkoani Kigoma, Col Marco Gaguti amewataka Viongozi wa Serekali na jamii Wilayani Buhigwe kuwatumikia Wanachi kwa nguvu zote na kuhakikisha uundwaji wa mfumo wa nyumba kumi.

Aidha Viongozi hao wa Serikali na jamii wametakiwa kukamilisha mara moja uundwaji wa mfumo wa kiutawala wa nyumba kumi ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na amnani katika wilaya hiyo.

“Ninatoa siku saba kukamilisha zoezi la kuhuisha daftari la kiusalama pamoja na uundwaji wa mfumo wa kiutawala wa nyumba kumi ambao utasaidia kwa kiwango kikubwa cha ulinzi na usalama wetu,”alisema Col. Gaguti.

Col Gaguti alibainisha hayo alipokuwa akiongea na Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya pamoja na Viongozi wa Serikali ngazi ya Wilaya katika kikao cha kujitambulisha kilichofanyika Julai 11,2016 katika ukumbi Wa Mikutano Wa Wilaya.

" Nataka kila Kiongozi ajipambambanue kwa kuwapigania na kuwatumikia wanachi,niwakati sasa wa kila mmoja wetu kuainisha kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka," alisema Col Gaguti.

Amewataka kuweka kipaumbele katika kukamilisha zoezi la upatikanaji wa madawati ya kushughulikia kero za wananchi.

Col Gaguti alisema  watendaji wa serikali kila ngazi wasimamie vyema shughuli za serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha lego la Serekali kutoa elimu bure yenye ubora lifikiwa mapema kwa kukamilisha mahitaji yote muhimu  na kusimamia huduma bora za Afya .
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti akisalimia baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili katika Ukumbi wa Hlamashauri kwaajil;i ya kikao cha kujitambulisha.
 Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Col. Marco Gaguti akisalimia baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo alipowasili katika Ukumbi wa Hlamashauri kwaajil;i ya kikao cha kujitambulisha.
 Akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya
watumishi wakimsikiliza mkuu huyo wa Wilaya. Source:Father Kidevu Blog

No comments: