Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Green Voices Tanzania uliofanyika katika
hoeteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata
maelezo namna ya mkaa wa karatasi unavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa
kampuni ya Mchau Windmill Ndugu Laurian Mchau wakati wa uzinduzi wa mradi wa
Green Voices Tanzania
Keki ya Muhogo
Mkaa wa karatasi
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakipata maelekezo ya namna zao la muhogo linavyoweza kuwa na idadi nyingi ya vyakula.
Mshauri na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Wanawake Barani Afrika Mhe. Getrude Mongella akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Green Voices Tanzania uliozindiliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
...........................
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza
watendaji wa Mradi wa Jukwaa la Kijani la wanawake Nchini wahakikishe
wanaendelea na mkakati wa kuelemisha wanawake kuhusu namna ya kukukabiliana na
mabadiliko ya Tabia hapa Nchi.
Makamu
wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati
anazindua mradi wa GREEN VOICES,mradi unaolenga kusaidia wanawake kukabiliana
na mabadiliko ya Tabia,unaofadhiliwa na
Rais wa Mfuko wa Wanawake Barani Afrika Maria Tereza Fernandes De la Vega
Makamu
wa Rais pamoja na kupongeza jitihada zinazofanywa na Jukwaa hilo katika
kusaidia wanawake kupambana na mabadiliko ya Tabia ya nchini, amesema bado upo
umuhimu mkubwa kwa wanawake kuelimishwa zaidi kuhusu mabadiliko hayo kwa sababu wao ni
moja ya kundi ambalo linaguswa na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwemo suala la ukame.
Amesema
bara la Afrika linapoteza mabilioni ya dola kutokana na mabadiliko ya Tabia ya
Nchi ikiwemo tatizo la ukame ambao umechangia kupunguza uzalishaji wa mazao ya
chakula na biashara kwa kiasi kikubwa pamoja na uhaba wa maji.
Makamu
wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema nchi za Afrika bado zinakabiliana uhaba wa kifedha,taarifa
sahihi na teknolojia katika jitihada za
kupambana ipasavyo na mabadiliko ya tabia ya nchini.
No comments:
Post a Comment