Tangazo

July 9, 2014

FASTJET KATIKA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA KATIKA VIWANJA VYA SABA SABA

Mmoja wa wateja wa Fastjet akipata maelezo ya huduma ya kununua Tikieti ya Ndege kupitia Mtandao wa simu
  Lucy Mbogoro, Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet. akitoa maelezo katika banda la Fastjet   “Fastjet ni shirika ambalo linatoa huduma za usafiri wa ndege kwa bei ya chini kabisa, daima tunawajali wateja wetu na ndio maana tumewasogezea huduma karibu na walipo”
 “Fastjet ni nzuri sana, ni watu wanaojali watu, wanawasikiliza, sielewi walitusikiliza sisi kama Wachungaji lakini kwa kweli ni waungwana sana” – alisikika Mchungaji John Kamwela pichani aliyekuja kukata tiketi kwa ajili ya safari yake na wachungaji wengine kuelekea kwenye mkutano.
 Roda Kayungi kutoka Fastjet akielezea  huduma ambazo wateja wengi wananufaika  nazo ikiwemo maelezo ya jinsi ya kulipia tiketi kwa njia ya simu pamoja na mtandao.

 Wateja wakipata huduma mbalimbali ikiwemo ukataji wa tiketi kwa bei za chini kabisa pamoja na fursa ya kufahamu kuhusu huduma za shirika la ndege la Fastjet ambalo kwa sasa ndege zake zinapaa kuelekea Dar es salaam, Mbeya, Kilimanjaro, na Mwanza

Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam maarufu kama Sabasaba jana yalifikia tamati katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es salaam.

Maonesho hayo yaliyoshirikisha mataifa zaidi ya 31 na makampuni zaidi ya 500 likiwemo kampuni bora la usafirishaji kwa njia ya anga ambapo kampuni hilo liliweza kuvutia idadi kubwa ya watu walio weza kutembelea na kunufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo punguzo la bei .

Watumiaji wa huduma za shirika la ndege la Fastjet maarufu kama Fastjetters walinufaika pia na kupata elimu namna mbalimbali za kuweza kukata tiketi /kufanya malipo kwa njia ya mtandao ili kuepusha foleni na gharama za watumiaji wa shirika hilo. 

Shirika la ndege la Fastjet limeweza kurahisisha usafiri wa anga na kuwafikia wananchi wa aina mbalimbali wenye kipato kikubwa na cha kawaida kuwaweka sawa fastjet ndege bora yenye nafuu kuliko ndege zote kwa usafiri wa uhakika na marubani makini.

No comments: