Hamisi Nassoro kutoka Carpet FC
akijaza fomu ya usajili kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars 2016 huku
akishuhudiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu wa mkoa wa soka wa
Temeke Kassim Ally
XXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Usajili wa wachezaji kwa ajili ya
mashindano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars 2016 umeanza leo
katika mikoa inayoshirikia michuano hiyo mwaka huu ambapo mashindano katika
ngazi ya mkoa yamepangwa kuanza wiki ijayo Julai 30.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na
Shirikisho la Mpira wa miguu nchi TFF, michuano hiyo ngazo ya mkoa inatarajiwa
kumalizka Agosti 28 na kufuatiwa na mashindano ya taifa yatakayofanyika jijini
Dar es Salaam kuanzia Septemba 6 hadi 11.
Akiongea wakati wa usajili katika
mkoa wa kisoka wa Temeke, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira Temeke Kassim Mustafa
alisema mkoa wake wamejiandaa vema kwa ajili ya kutetea ubingwa walioshinda
mwaka jana. “Leo tumeanza usajili wa wachezaji kwa ajili ya michuano ya Airtel
Rising Stars 2016. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Airtel kwa mradi wake
huu wa kusaka na kukuza vipaji vya soka kwa vijana wetu. Temeke tunao vipaji
vyingi na ndio sababu mkoa wetu uliweza kushinda taji la ARS 2015,” alisema
Mustafa.
Naye kocha mkuu wa Twalipo Youth
Academy Neville Kanza alisema anafurahi ujio wa Airtel Rising Stars 2016 huku
akisema vipaji vipo vingi na kutamba kuendelea kutoa vijana wengi kwenye
kombaini timu ya mkoa. Mwaka jana Twalipo academy ilitoa wachezaji watano ambao
waliunga timu ya taifa ya Airtel Rising Stars Dream Team.
Kwa wake Ofisa Uhusiano Airtel
Tanzania Jane Matinde alisema wanayo furaha kuona vijana wameweza kufanikisha
ndoto zao kwa kupitia michuano ya Airtel Rising Stars. “Ni furaha kuona timu
zetu za taifa zikiwa na wachezaji ambao wametoka na program hii ya Airtel
Rising Stars,” alisema na kuongeza kuwa hii ni fursa nyingine kwa vijana
kujitokeza kwenye usajili ambao utawawezesha kushiriki michuano hii na
kuonyesha vipaji vyao.
Alisema Airtel Rising Stars mwaka
inafanyika chini ya mwanvuli wa kampeni ya Airtel RURSA iliyozinduliwa mwaka
jana kwa lengo la kuwahamasisha vijana kutumia fursa mbalimbali walizonazo ili
kujiendeleza kiuchumi. “Airtel Rising Stars yenyewe ni Airtel FURSA kwa kuwa
inawawezesha vijana kutumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha kupitia mpira.
Mpira ni chano cha kipato cha kuaminika”, alisema.
Mikoa inayoshirikia mwaka huu
ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mwanza, Mbeya na Morogoro (wavulana) na
Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Lindi na Zanzibar zikishirikisha wasichana.
No comments:
Post a Comment