Tangazo

December 29, 2011

Mtangazaji wa TBC -Taifa, Halima Mchuka afariki Dunia

Halima Mchuka (kushoto) enzi za uhai wake.
MTANGAZAJI wa muda mrefu wa iliyokuwa  Redio Tanzania Dar es Salaam RTD  na baadae Shirika  la  Utangazaji  Tanzania (SHIUTA) amefariki Dunia. 

Taarifa zilizopatikana  hivi  punde zinadai  kuwa Mtangazaji  huyo  ambaye  alikuwa na  kipaji  kikubwa cha  utangazaji amefariki  Usiku  huu  wa  leo  tarehe  29-12-2011 saa 9.00alfajiri  kutokana  na kupatwa  na  stroke ya  ghafla  .
 
“Alikuwa  na tatizo  hilo  jana mchana mara baada  ya kutangaza kipindi  cha salaam cha  TBC-Taifa na akazidiwa ndipo  alipopelekwa  Hospitali  na sasa  ndiyo amefariki  dunia.”alibainisha mmoja wa watangazaji wa TBC ambaye  alikuwa jirani  na mtangazji  huyu.

 Halima Mchuka inaaminika  kuwa  alijiunga  na Radio  Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi  katika idara ya  Habari na idara   ya Mipango.

Wadau  wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili  kwa  kuwa  mwanamke wa awali  kuangaza mpira  katika  ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki  na  Kati.

“Unapotaja mpira wa miguu wakai huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu  dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wachezaji nguli wa  Tanzania wa wakati huo.

Kwa hakika  si  wasikilizaji  wa  RTD na wanamichezo tu  bali  ata  watu wa Karibu  ambao  waliwahi  kufanya nae  kazi     tunamtazama kuwa  ni  mtu mpole  mwenye  huruma  na  kusaidia  wenzake pale  penye tatizo  ambalo  yeye  anaweza kulitatua.

”unajua  huyu  mama  mimi ndiye aliyenisaidia  kuweza kupata  kazi  kwenye taasisi  hii  nilikuwa wala  simfahamu  mtu ,amenisaidia sana.”kuficha  ni  dhambi  alinidokeza mfanyakazi mmoja wa SHIUTA.

Mara  ya  mwisho kuongea  na  mwana mama  huyu nilikuwa nikiwa Iringa alinipigia simu na kuniulizia taarifa  za  familia  yangu  na kuniambia  nimtunze sana  mtoto  wangu  lakini   huku akiniambia  na kutambua “ mbona leo unaongea  kwa unyonge” ah “ Halima  hapana  ila nipo  eneo  ambalo  watu  wanasoma ndiyo  maana  naongea  kwa sauti ya  chini “nilimjibu wakati huo  kwani nilikuwa makaba ya  Chuo Kikuu  cha  Tumaini Makumira- Iringa.
 
Mungu  ailaze Roho ya Bi. Halima Mchuka pahala pema peponi Amina

No comments: