Moja kati ya wajasiriamali watakaokuwepo katika maonyesho ya
wajasiriamali ya Airtel FURSA, Bi. Theresia Maliatabu akiandaa bidhaa zake za
picha za Sanaa nyumbani kwake mbagala rangi tatu. Theresia ni moja kati ya
wafanyafanya biashara waliowezeshwa na mradi wa kuinua vijana wa Airtel
FURSA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM
Mkuu wa
wilaya ya Kinondoni, Mh. Ally Hapi anatarajiwa kufungua maonyesho ya
wajasiliamali mbalimbali wanaodhaminiwa na Mpango wa
Airtel FURSA yatakayofanyika ijumaa hii katika viwanja vya ofisi za
Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi
jioni.
Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA tunakuwezesha, umeandaa mpango utakaowawezesha wajasiriamali
hao ambao awali waliowazezwa kupitia mpango wake wa Airtel FURSA ili
waweze kuonyesha biashara zao kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara
kutangaza na kupata masoko ya biashara zao ili kukuza biashara na
mitaji yao.
Akiongea juu ya maonyesho hayo, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson
Mmbando alisema “ tumeonelea ni vyema kujipanga katika kuendeleza dhamira yetu
ya kuwainua vijana na kuhakikisha mpango huu wa Airtel FURSA unaleta tija na
kuinua biashara zao. Watakaoshiriki ni zaidi ya wafanyabiashara 28 na
vikundi vinne vilivyonufaika kwa kupatiwa vitendea kazi kupitia mradi
wetu wa Airtel FURSA ambao kwa sasa wanafanya vizuri katika biashara zao”.
Airtel tumeona ni vyema tukiendelea kuwawezesha kwa kuwatafutia masoko
endelevu ndani na nje ya nchi kwa kuwashirikisha katika maonyesho haya yenye
lengo la kutangaza biashara zao na kupata masoko zaidi, tunatoa wito kwa
watanzania kuwaunga mkono kwa kufatilia kazi zao kupitia mitandao ya kijamii na
kupata fursa ya kutembelea maonyesho haya siku ya kesho.
Bidhaa zitakazo kuwepo katika maonyesho hayo ni pamoja na Sanaa za picha
za ukutani, vifaa vya magari, vyakula mbalimbali kama matunda ,korosho, cake,
mifugo kama vile kuku wa kisasa, bidhaa za kiafrika, mapambo ya nyumbani
na kadhalika.
No comments:
Post a Comment