Tangazo

October 31, 2016

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA TAMASHA LA MAZINGIRA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI KATIKA UKUMBI WA NKRUMAH UDSM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah Hall,tayari kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wajumbe walihudhuria mkutano wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.                    


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikikata utepe kuashiria kuzindia kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wengine kuonyesha juu kitabu cha Pastoralism and Climate Change in East Africa kuashiria kimezinduliwa rasmi kwenye Tamasha la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia Nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika ukumbi wa Nkurumah Hall, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
                                 ..........................................................................
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku uharibifu mkubwa wa mazingira unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambao unaweza kusababisha nchi kugeuka jangwa.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira
chini ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ameonya kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke yake bali ni kila mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo wananchi ni muhimu kwa umoja wao wakaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na hali tete ya uhabifu wa mazingira nchini.
“Uharibifu wa mazingira usimame leo na marekebisho ya uharibifu tulioufanya uanze leo na hili ni jukumu la kila Mtanzania”
Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa viongozi wa ngazi zote nchini kuchukua hatua katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo yao ili visitoweke.

Makamu wa Rais ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza kuleta athari si kwa Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa zinakabiliwa ipasavyo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya Tabia ya nchi,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Pius Yanda amesema mkutano huo wa siku TANO utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. 


No comments: