Tangazo

October 24, 2016

TIGO YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI WILAYA YA USHETU

Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kwa kanda ya Ziwa Ali Maswanya( fulana ya Blue) akimkabidhi kisima cha maji Mwenyekiti wa kijiji cha Ulowa 4 Hamad Mohamed kisima cha maji kilichojengwa na mtandao huo,wilayani Ushetu Mkoani Shinyanga.Kina thamani ya shilingi milioni16 /-.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kwa kanda ya Ziwa Ali Maswanya(wa pili kulia) na mkazi wa kijiji cha Ulowa 4 wilayani Ushetu mkoani Shinyanga Magreth Charles wakikamua maji kwenye kisima kilichojengwa kijijini hapo na mtandao huo chenye thamani ya shilingi milioni16/- , wakati wa Uzinduzi.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kwa kanda ya Ziwa Ali Maswanya akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Ulowa 4 Magreth Charles, wakati wa uzinduzi wa kisima wilayani Ushetu Mkoani Shinyanga.
Meneja Masoko wa Tigo kwa kanda ya Ziwa Ali Mashauri,akimtua ndoo ya maji  mkazi wa kijiji cha Ulowa 4 wilayani Ushetu mkoani Shinyanga Tatu Kapembe,wakati wa uzinduzi wa kisima cha maji kijijini hapo.

No comments: