Tangazo

October 14, 2016

UMOJA WA MATAIFA WAFIKISHA MALENGO YA DUNIA MKOANI SIMIYU

UMOJA wa Mataifa nchini Tanzania unaendelea na uelimishaji wa wananchi kuhusu malengo ya Dunia yaliyoelezwa katika Maendeleo Endelevu (SDGs), malengo ambayo sasa yana takribani mwaka mmoja.

Ili kuweza kufikisha malengo hayo kila mahali , Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali utatumia wiki ya vijana kufundisha wanafunzi 400 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Simiyu ili wawe wakufunzi kwa wenzao.

Mafunzo hayo yamelenga kuwafanya vijana kuelewa na kuongeza ufahamu kuhusiana na malengo hayo ya dunia, hivyo kuwasaidia wenzao na wananchi wengine kutambua wajibu wao katika utekelezaji wake.

Mafunzo hayo mkoani Simiyu ni mwendelezo wa mafunzo yaliyozinduliwa mkoani Arusha na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.

Hadi sasa Umoja wa Mataifa umewezesha vijana 70 kutambua malengo hayo na kutumika kufunza wengine. Aidha wabunge zaidi ya 180 walipewa mafunzo hayo huku wahadhiri na wanafunzi 1,000 kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakiwa nao wamenolewa kuhusiana na malengo hayo ya maendeleo endelevu.
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja huo hapa nchini kwenye mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu, yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia umaskini, sera na uchambuzi, Bw. Mudith Cheyo alichangia katika mafunzo hayo kwa kueleza ni kwa namna gani serikali inatekeleza malengo hayo ya dunia. Bw. Cheyo amesema “Asilimia kubwa ya nguvukazi ya taifa letu ni vijana hivyo basi ni muhimu sana kuwashirikisha katika utekelezaji wa Malengo Ya Dunia katika ngazi ya taifa. Asilimia 34 ya nguvu kazi ni vijana, serikali imepanga mikakati kuhakikisha vijana wanapewa uwezo wa kuwawezesha kuzitumia fursa zilizopo kuleta maendeleo.”

Alisema kwamba kuwafunza vijana kuhusu malengo hayo ya maendeleo endelevu ni sehemu ya utendaji wa serikali katika utekelezaji wa malengo.

Akizungumza katika semina ya malengo endelevu, Bw.Amon Manyama, Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja huo(UNDP), alisema ajenda ya maendeleo kuelekea mwaka 2030 inahitaji ushiriki wa kila mmoja wetu hasa vijana.
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Didi Nafisa akitoa utangulizi wa Malengo ya Dunia (Global Goals) kwa kundi la vijana wa Simiyu (hawapo pichani) katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.

“Ni muhimu sana kwa vijana kuelewa Malengo ya Dunia. Huu ni wakati wao. Kwa kuyaelewa malengo haya inrahisisha utekelezaji wake. Nimefurahi kuona muamko wa vijana waliojitekeza hapa leo na natumaini watawafikishia wengine ujumbe huu.” alisema na kuwapongeza vijana hao 400 kwa ushiriki wao katika kujifunza na kuelewa malengo hayo ya dunia na wajibu wa kila mmoja wetu.

Septemba 2015, viongozi 193 kutoka nchi mbalimbali duniani walikubaliana kuhusu malengo endelevu 17 kuelekea mwaka 2030.
Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akiwapiga msasa wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) vijana wa mkoa wa Simiyu wakati wa mafunzo ya siku moja yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Malengo hayo ambayo yanatakiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 14 ijayo yanaleta kwa pamoja shughuli za kijamii, kiuchumi na kimazingira ili kuwa na maendeleo endelevu.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yakifanya kazi chini ya mwavuli mmoja yanasaidia serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kwamba inafanikiwa katika kuyaingiza malengo yote 17 katika mpango wake wa maendeleo wa mwaka 2025 kupitia mpango wake wa kuisaidia Tanzania (UNDAP ll) ulioanza mwaka huu hadi mwaka 2021. Kwa bahati UNDAP II unaenda sanjari na mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka mitano wa 2016-2021. (FYDP II)
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mudith Cheyo akieleza ni namna gani serikali inatekeleza Malengo ya Dunia na kuwata vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kuyaelewa vyema na kuwa mabalozi kwa jamii zao na vijana wenzao ili utekelezaji wa malengo hayo yafanikiwe kwenye mafunzo ya siku moja kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mudith Cheyo akisisitiza jambo kwenye mafunzo.
Pichani juu na chini ni umati wa vijana wa Simiyu uliohudhuria mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.




Afisa Ardhi Mtathmini kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu, Lazaro Magumba, akiuliza swali kwa wawezeshaji kutoka Serikalini na Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Guduwi Bariadi, Seif Masoud akishiriki kwenye mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwanafunzi wa SAUT-Mwanza Hatibu Hamisi ambaye pia ni mwanachama wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) akieleza vijana wenzake (hawapo pichani) juhudi na maarifa aliyotumia kutunga kitabu cha 'Wanawake na Haki Zao' ambacho anapanga kutokiuza bali kielimishe jamii ya Watanzania kuhusu haki za msingi za wanawake wakati mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mwanafunzi wa SAUT-Mwanza Hatibu Hamisi (kushoto) ambaye pia ni mwanachama wa Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA), akikabidhi kitabu hicho kwa Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama katika mafunzo ya siku moja kwa vijana wa Simiyu yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Ofisa wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Didi Nafisa (kulia) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo Vikuu, Zenda Daniel wakati wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mchekeshaji maarufu wa mkoa wa Simiyu anayefahamika kwa jina la Madodoso a.k.a Handsome boy wa Simiyu akitoa burudani kwa vijana wakati wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya UN na kufanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Mchekeshaji maarufu wa mkoa wa Simiyu anayefahamika kwa jina la Madodoso a.k.a Handsome boy wa Simiyu (kulia) akimvunja mbavu Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama alipokuwa akitoa burudani kwa washiriki wa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Alliance mjini Bariadi mkoani Simiyu.
Vijana wakiangua vicheko ukumbini hapo.

Sehemu ya washiriki wakiwemo walimu wa shule mbalimbali walioambatana na wanafunzi wao.

Baadhi ya vijana katika picha ya pamoja na mabango ya malengo ya dunia mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku moja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa vijana wa mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliokuwa mkoani Simiyu kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa katika picha ya pamoja wakiwakilisha malengo ya dunia.

No comments: