Mkuu wa Masoko na Hazina wa
BancABC, Barton Mwasamengo, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na
wafanyabiashara wadogowadogo, Joyce Malai, wakionyesha kadi inayoonyesha
uzinduzi wa ofa ya riba asilimia 16% kwa wateja wanaofungua akaunti ya amana ya
muda maalum msimu huu wa sikukuu, katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika makao makuu ya BancABC jijini Dar es Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
BancABC yatoa ofa kabambe ya riba
hadi 16% kwa wateja wanaofunga akaunti ya amana ya muda maalumu msimu huu wa
sikukuu.
Benki ya ABC ambayo ni sehemu ya
Atlas Mara imekuja na ofa maalumu kwa ajili ya wateja msimu wa sikukuu, ambapo
wateja watakao fungua akaunti ya amana na kuweka pesa kuanzia milioni 10 kwa
muda maalum atafaidika na ofa hii yakupata riba ya juu kuliko zote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,
Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na wafanya biashara wadogo wa Benki ya ABC
Bi Joyce Malai alisema tunaatoa riba ya hadi 16% kwa mwaka na kwamba watalipwa
riba papo kwa papo ikiwa ni zawadi yao msimu huu wa sikuku.
“Hii ni ofa bora kuliko zote
kwenye soko kwa sasa na tunataka kuwashawishi wateja wetu na hata wale
wasiokuwa na akaunti kwetu kutumia fursa ya ofa hii ya msimu huu wa sikukuu,”
alisema.
Mkuu wa Idara hiyo ya
Benki ya ABC alisema wana nia ya kufikia mahitaji ya wateja na kuhakikisha
kwamba wanakua pamoja na benki hiyo. “Tunathamini jinsi wateja wetu
wanavyotuunga mkono na hiyo ndio sababu sisi kama benki tumeamua kuwazawadia
ofa hii kabambe katika msimu huu wa sikukuu,” alisema.
“Kinachotakiwa kufanywa na mteja
yeyote ili aweze kujipatia ofa hii nikufika kwenye tawi letu lolote – Uhuru,
Quality Centre, Kariakoo na Arusha, afungue akaunti ya amana ya muda maalumu
ambapo riba hiyo italipwa papo hapo, lengo ni kukupa uhuru wa kuitumia kwa
ajili ya kufanya manunuzi binafsi kama upendavyo ikiwemo kununua
zawadi kwa familia au marafiki ili kuwaongezea furaha katika msimu huu wa
sikukuu,” alisema.
Aliendelea kusema kwamba ofa hiyo
itawahusu wateja watakaofungua akaunti za amana za muda maalumu na Benki ya ABC
Kabla ya Desemba 31, ikimaanisha kwamba ofa hiyo itakuwa halali kwa msimu wa
sikukuu tu.
“Tunataka msimu huu wa sikukuu
kuwa mzuri zaidi kwa wateja wetu kwa kuwa tunafahamu kwamba watu wengi hutumia
kiasi kikubwa cha fedha wakati wa Krismasi. Kupitia riba hii watakayopata
awali, wataweza kupata mahitaji yao kirahisi,” alisema.
No comments:
Post a Comment