Tangazo

January 17, 2017

KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO WA KATA YA IGOMBAVANU NA IKWEA ZAPAMBA MOTO

 
Mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati akimpigia kampeni mgombea udiwani wa kata ya Igombavanu na kuwataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
 katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo
 Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo
Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho 

Na fredy mgunda,Iringa

MBUNGE wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati amewataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
 
Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Makongomi mbunge Kabati aliwaambia wananchi kuwa jimbo la Mufindi kaskazini na wilaya ya Mufindi kwa ujumla ni ngome ya chama cha mapinduzi (CCM) hivyo wapinzani wasipoteze muda wa kupiga kampeni kwa kuwa hawawezi kushinda chaguzi zote za jimbo hilo.

Kabati alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Mufundi bado wanakipenda chama cha mapinduzi na wanahakika watashinda kutokana na mapokeo mazuri kutoka wapiga kura ambao wanazikubali sera za chama cha mapinduzi na wanaendelea kumuamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mimi nikiangalia naona nyuso za furaha tu hapa na nimepemda kuwa mmetukikishia kushinda uchaguzi huu basi furaha yangu itakuwa siku ile diwani wetu kutoka chama cha mapinduzi anatangazwa kuwa mshindi kwa kura nyingi,nawapenda na naomba mkipe kura nyingi chama cha mapinduzi”.alisema Kabati 

Naye mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo.

“Jamani nipeni huyu diwani ili tuendelee kufanya maendeleo kwa kuwa mimi mnaniamini basi naomba mpeni kura nyingi na kuondokana na maneno machafu kutoka kwa wapinzani kwani wapinzani hawana jipya saizi”.alisema Mgimwa 

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo,alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Rashidi Mkuvasa kwa kuwa ni kiongozi mzuri na atawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo.

“Tumeona wagombea wengi wakija hapa kupiga kampeni na kuomba kura kwa njia ya matusi na kuhamasisha kutomchagua kiongozi furani pasipo kutaja au kuongelea hata hoja za msingi kwanini wanaomba kura zetu” alisema Mhagama

Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho au kunakili namba za vitambulisho hivyo
.
“Tuwakatae viongozi wa namna hiyo kwa kuwa lengo lao ni kutaka kununua uongozi kwa nguvu ya pesa na kuwa wao sio chaguo la wanachi hivyo wananchi msithubutu kufanya hivyo mtapoteza haki yenu ya msingi na hamtampata kiongozi atakaye waletea maendeleo”.alisema Mkuvasa

Aidha wananchi wa kata ya Igombavanu katika jimbo la Mufindi Kaskazini wamempongeza mgombea udiwani wa kata kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Rashidi Mkuvasa kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuwapa matumaini kuwa atakuwa kiongozi mzuri na kuwaletea maendeleo katika kata hiyo.

No comments: