Jonathan Tarimo (kushoto) kijana mjasiriamali
anayejishughulisha na ufugaji akimwonyesha Afisa Masoko Airtel mkoa wa
Arusha, Geoffrey Sayore ndama wa mmoja wa ng’ombe aliyewezeshwa na Airtel
kupitia mpango wake wa Airtel FURSA, wakati alipomtembelea ili kujionea
maendeleo yake katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
ARUSHA
Vijana wanaojishughulisha na
ujasiriamali wametakiwa kutokata tamaa na matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo
wakati wa shughuli zao.
Wito huo umetolewa na mfugaji Jonathan Tarimo, mkazi wa mkazi wa Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha anayejishughulisha na ufugaji
Kijana huyo miezi mitano iliyopita aliwezeshwa kupitia mpango wa Airtel FURSA msimu wa pili kwa kupatiwa ng’ombe wawili, banda la kisasa na mafunzo ya biashara.
Akiongea na maofisa wa Airtel
waliotembelea katika mradi wake wa ufugaji ili kujionea maendeleo ya biashara
yake alisema kwamba amepata matatizo katika shughuli yake baada ya
ng'ombe aliyekuwa anampa maziwa kufa.
“Nawashukuru sana Airtel kwa
kunisaidia kufikisha hapa nilipo sasa, maana nlikuwa na ngo’mbe mmoja tu na
Airtel kupitia Airtel Fursa kwa kunipatia ngombe wawili ambapo mmoja alizaa na
nikawa nauza maziwa kwa wingi lakini baadae alifariki kutokana na ugonjwa.
Kwahiyo nikawa nimebakiwa na ng’ombe wawili na ndama. Kwa sasa ndama anaendelea
vizuri na huyu ngo’mbe mwingine niliyewezeshwa anamimba. Kwasasa changamoto
kubwa ni kutafuta chakula kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nimekuwa
nikienda umbali mrefu ili kupata chakula cha mifugo yangu”.
Alisema, pamoja na adha
aliyoipata, aliwaasa vijana wenzangu tusikate tamaa na kuendelea kutafuta fursa
mbalimbali zitazoweza kufikisha katika malengo yao hata kama wakipata
changamoto mbalimbali
Naye Afisa masoko Airtel mkoa wa
Arusha Geoffrey Sayore alisema, Jonathan amekuwa ni mfano mzuri wa kijana
aliyewezeshwa na Airtel FURSA na kuweza kupiga hatua kwenye biashara yake
pamoja na changamoto mbalimbali zinazomzunguka.
Aliwataka vijana wanapopata
fursa waweze kuzitumia vizuri ili ziwasaidie kuongeza kipato na kutoa ajira kwa
jamii inayowazunguka. Lengo letu sisi Airtel ni kuhakikisha vijana wanafaidika
na mradi huu wa Airtel Fursa na ndio maaana tunafanya ziara hii kutadhimini
mafanikio, changamoto na maeneo ya kuwawezesha zaidi ili kuzifikia ndoto zao
na kuwawezesha vijana wengi zaidi.
Airtel FURSA ni mradi wa kijamii
kutoka Airtel Tanzania wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali kwa
kuwapatia vitendea kazi na elimu ya ujasiriamali ili kuboresha biashara zao.
No comments:
Post a Comment