Naibu Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kufanya ukaguzi wa mazingira katika eneo la kiwanda cha unga wa ngano
cha Azania kilichopo Ubungo jijini Dar Es Salaam jana.
|
Akiendelea na ziara yake ya ukaguzi
na utekelezaji wa sheria ya Mazingira jijini Dar es Saalaam, Naibu Waziri Ofisi
ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameagiza Baraza
la taifa la Usimizi wa Mazingira NEMC
kwa kushirikiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa Ngano wa Azania,
kupima kiwango cha ubora wa hewa inayoambatana na vumbi la unga wa ngano
linalotoka kiwandani hapo baada ya shughuli za uzalishaji na kwenda kwenye mazingira na makazi ya watu
kana vinakidhi viwango vya kimazingira.
Mpina alisema kuwa baada ya matokeo
hayo yanayotegemewa kutoka baada ya wiki
mbili, serikali ndiyo itakuwa kwenye hatua ya kusema jambo kwa wananchi pamoja
na kiwanda.
“Baada ya matokea hayo sasa serikali
inaweza kuwa na nafasi ya moja kwamoja kuchukua hatua kwa mwenye kiwanda ikiwa
ni pamoja na kukitoza faini kwa mujibu wa sheria, na kama matokeo ya vumbi na
kelele zitokazo kiwandani hapo yatakuwa ndani ya kiwango, sasa hatua
itakayofuata ni yakuangalia mahusiano kati ya mwenye kiwanda na wakazi majirani
wa eneo hilo. Alisema Mpina.”
Aidha Mpina aliongelea kufaanyika kwa
taratibu za kujua kama suala la kiwanda hicho kuwa karibu na makazi ya watu
, ni sahihi na kwa upande wa wananchi
kuwa karibu na kiwanda hususan kuwepo
kwa nyumba kila baada ya hatua moja nalo ni sahihi.
Awali katika muendelezo wa ziara yake ya ufuatiliaji
na utekelezaji wa sheria ya mazingira jijini Dar es Salaaam, Naibu Waziri Mpina
alikitembelea kiwanda cha Chemi cotex kilichopo Mbezi Beach.
No comments:
Post a Comment