Tangazo

March 7, 2016

Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), yaendesha semina kwa Wanawake Wajasiriamali

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), Rebecca Stanford (kushoto), akiwaonesha nguo wanawake wajasiriamali katika semina ya siku moja ya kuwaongezea uwezo na stadi za maisha iliyofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Taasisi hiyo Ukonga jijini Dar es Salaam.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa kwenye semina hiyo.
 Semina ikiendelea.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), Rebecca Stanford akionesha viatu vinavyotengenezwa na wajasiriamali hao.
 Mwezeshaji wa Taasisi hiyo, Harun Sabil Baluchstan (kulia), akiendesha mafunzo kwa wajasiriamali hao.
Semina ikiendelea.

Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE wametakiwa kuwa na moyo wa kuthubutu ili kujiletea maendeo badala ya kukaa bure bila kazi jambo litakalo waondoa katika maisha ya utegemezi.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), Rebecca Stanford wakati akizungumza na wanawake wajasiriamali katika semina ya siku moja ya kuwaongezea uwezo na stadi za maisha iliyofanyika Ukonga Dar es Salaam Jumamosi.

"Kuna fursa nyingi ndani ya ujasiriamali hivyo mnapaswa kuthubutu kwa kubuni vitu mbalimbali kama utengenezaji wa nguo, viatu, ufugaji, urembo na vingine vingi badala ya kusubiri kupewa" alisema Stanford.

Akizungumzia kuhusu taasisi hiyo, Stanford alisema wamejikita zaidi katika kushirikisha jamii, wahisani, wadau wa maendeleo ikiwemo Serikali kupigania ustawi wa kiuchumi, kijamii na kiutamaduni ili kuondoa umaskini, unyanyasa na uonevu kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu.

Aliongeza kuwa Shirika hilo si la kisiasa, kidini wala kibiashara na limeundwa kwa nia ya kuhudumia na kusaidia jamii na limesajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 na kupata namba ya usajili 00NGO/08289.

No comments: