Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akionyesha nambari ya smati kadi ya mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Wakishuhudia tukio hilo ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Bi. Chiku Salehe (kulia). Katika droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akionyesha nambari ya smati kadi ya mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Wakishuhudia tukio hilo ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Bi. Chiku Salehe (kulia). Katika droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (wa kwanza kulia) akimpigia simu mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Wakifuatilia tukio hilo kutoka kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Bi. Chiku Salehe, mfanyakazi wa StarTimes kutoka kitengo cha maudhui, Bw. Daniel Msangi na Meneja Uhusiano, Bw. Muddy Kimwery. Katika droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (kushoto) akimpigia simu mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Wakifuatilia tukio hilo kutoka kulia ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania, Bi. Chiku Salehe, mfanyakazi wa StarTimes kutoka kitengo cha maudhui, Bw. Daniel Msangi na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka. Katika droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (wa kwanza kulia) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa tano na wa mwisho wa safari ya kwenda Ujerumani. Katika droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo cha Sport Plus.
Meneja Mauzo wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa droo ya tano na ya mwisho ya safari ya kwenda Ujerumani. Katika droo hiyo pia StarTimes walitangaza ofa ya punguzo la bei kipindi hiki cha Pasaka kwa kushusha bei ya visimbuzi pamoja kufurahia vifurushi vya kawaida na cha michezo cha Sport Plus. Akimsikiliza kwa makini kulia ni Meneja Uhusiano, Bw. Muddy Kimwery.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni ya StarTimes imezindua ofa bab-kubwa kwa wateja wake wote nchini kwa kushusha bei ya visimbusi vyake vya antenna na dishi pamoja na kuwapatia ofa ya kutazama kifurushi cha michezo cha Sport Plus mwezi mmoja bure kabisa.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo ulioambatana na uchezeshwaji wa droo ya mwisho ya kusijishindia safari ya Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka ameeleza kuwa ofa hiyo ni maalum kusindikiza shamrashamra za sikukuu za Pasaka.
“Leo nina habari njema kwa wateja wetu kwamba kuisha kwa promosheni ya kujishindia tiketi ya kusafiri Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga ‘live’ imefikia ukingoni siku ya leo. Ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza mshindi wetu wa mwisho Bw. Makame Kundi Makame kutoka visiwani Zanzibar na kutufungia pazia ya promosheni hiyo. Lakini kama tulivyokwisha waahidi wateja wetu kwamba mwisho wa promosheni hii ni mwanzo wa promosheni nyingine ya Pasaka.” Alisema Bw. Kisaka
“Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye shamrashamra za Pasaka tungependa kuwataarifu wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa tumeshusha bei ya visimbuzi vyetu. Vya antenna vitapatikana kwa shilingi 22,000/- tu pamoja na mwezi mmoja wa bure wa vifurushi vya Mambo na cha michezo cha Sport Plus. Na wateja wa dishi watajipatia kwa shilingi 46,000/- pamoja na mwezi mmoja wa kifurushi cha Smart na Sport Plus.” Aliongezea Bw. Kisaka
Meneja huyo wa Masoko amefafanua kuwa ofa hizo ni kutaka kuwaonyesha ni jinsi StarTimes imejizatiti kwa chaneli na vipindi vya michezo hususani mchezo wa soka unaopendwa na watanzania wengi. Kwa kupitia punguzo hilo la bei anaamini kuwa sasa huduma zao zitapatikana kwa urahisi na kufurahiwa na kila mtu.
“Kupitia ofa ya mwezi mmoja ya kifurushi cha Sport Plus chenye chaneli za Sport Life, Sport Premium na Worl Football zinazoonesha ligi za Bundesliga na Serie A moja kwa moja ninaamini Pasaka hii itakuwa ni shangwe tupu. Kwa wateja wetu ambao tayari wanavyo visimbuzi vya antenna na dishi pia hatujawasahau kwani wao wakilipia vifurushi vya mwezi vya Mambo na Uhuru pamoja na Smart watapata mwezi mmoja bure wa kifurushi cha Sport Plus na vile vile watakaolipia vifurushi vikubwa va Kili na Super watapatiwa wiki moja zaidi ya vifurushi hivyo.” Aliongezea Bw. Kisaka
“Ningependa kuwapongeza washindi wetu wote waliojipatia fursa ya kushinda safari ya Ujerumani, ninaamini watafurahia safari yao. Pia ningetoa wito kwa wateja na watanzania kwa ujumla waichangamkie fursa hii ya punguzo la bei na kufurahia mechi za Bundesliga na Serie A kupitia kifurushi cha Sport Plus. Kwa bei ya sasa ninaamini hakuna atakeyekosa kisimbuzi chetu wala kutofurahia mechi hizo za ligi za Ulaya.” Alihitimisha Meneja huyo
Mshindi katika droo hiyo mwisho, Bw. Makame Kundi Makame mwenye umri wa miaka 43 ni mkazi wa Unguja visiwani Zanzibar na anajishughulisha na shughuli za hotelini.
Akizungumza kwa njia ya simu alisema kuwa amefurahishwa sana na promosheni hiyo kwani mara nyingi kampuni zingine huwahusisha wateja wao waliopo Dar es Salaam pekee. Lakini mpaka yeye kupigiwa simu alisema kweli kwa hakika StarTimes iliposema promosheni hiyo ni kwa wateja wao wan chi nzima ilikuwa ikimaanisha.
Bw. Makame anaungana na washindi wengine wanne waliopita ambao ni Profesa Bernadeta Killian wa Iringa, Bi. Kisa Uswege wa Mbeya, pamoja na Bw. Yohanes Maluli na Bw. Joseph Mogela wote wa jijini Dar es Salaam. Hivyo baada ya droo hiyo kukamilika washindi hao wanasubiri safari yao ya kwenda Ujerumani ambayo inatazamiwa kuwa mwezi ujao wa Aprili.
No comments:
Post a Comment