Tangazo

July 27, 2011

Buriani Kaka Danny Mwakiteleko


Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda  ambaye pia alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Danny akiwa na watoto wa marehemu, Caroline (kulia) na Vanesa  wakielekea makaburini.

Jeneza lenye mwili wa Danny likiteremshwa kaburini kwa maziko.

Mke wa Marehemu Danny Mwakiteleko akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu mume wake.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jackson Msome akiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu Danny Mwakiteleko mara baada ya mazishi.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ambaye pia ni mhariri wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda pamoja na wahariri wengine na wanahabari wakilia kwa majonzi makubwa mara baada ya kuupumzisha mwili wa Marehemu, Danny Mwakiteleko.PICHA: www.fullshangwe.blogspot.com

No comments: