Tangazo

July 27, 2011

Dancer wa Twanga Pepeta 'Baby Tall ' afanyiwa Kitchen Party leo kufunga ndoa na Dancer mwenzake 'Super K'

Mnenguaji mahiri wa Bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Betty Jonson Mwangosi (Baby Tall), akiingia ukumbini wakati wa sherehe yake ya Jikoni 'Kitchen Party' iliyofanyika jana usiku katika Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, ikiwa ni maalum kwa ajili ya kumuaga na kumfundisha mambo kadhaa kuhusiana na Ndoa.
Sherehe hiyo iliratibiwa na wanenguaji wenzake wa Twanga ikiongozwa na Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka huku ikisimamiwa kwa karibu kabisa na Kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu, huku ikihudhuliwa na wanamuziki na mashabiki lukuki wa bendi hiyo pamoja na baadhi ya watangazaji wa Redio.
Lilian Internet, akiwamiminia kinywaji cha Shampen, Bi Harusi mtarajiwa na mpambe wake.
Baadhi ya wageni waalikwa wakigonganisha grasi, ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Bi Harusi mtarajiwa.
Mshereheshaji wa Sherehe hiyo, Mai Martha, akiendesha shughuli hiyo.
 Luiza Mbutu, akitoa maneno ya kumuhasa Bi Harusi.
Wanenguaji wa Twanga wakisasambua.

No comments: