Tangazo

August 25, 2011

Wanafunzi IMTU wakabiliwa na matatizo ya Kitaaluma

Rais wa  Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha TIBA (IMTU), Yeredi Chacha (kushoto) akiongea  jijini Dar es Salaam leo katika mkutano wa viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha TIBA (IMTUSO) kuzungumzia matatizo mbalimbali yanayowakabili wanafunzi wa chuoni hapo mbele ya waandishi wa habari. Kulia ni Rais Mstaafu wa chuo hicho,  Jonas Mushi. PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO
Rais mstaafu wa  Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha TIBA (IMTU),  Jonas Mushi akionyesha baadhi za nyaraka za Mikataba  ya chuo na wanafunzi wakati viongozi wa jumuiya ya wanafunzi wa chuo kikuu cha TIBA (IMTUSO) walipokutana  na waandishi wa habari kuzungumzia matatizo mbalimbali ya kitaaluma yanayoendelea kukabili wanafunzi wa chuo hicho. Kulia ni Waziri Mkuu wa Serikali hiyo, Daniel Msafiri.
Waziri Mkuu wa Serikali ya chuo kikuu cha TIBA ( IMTU), Daniel Msafiri akisistiza jambo mbele ya waandishi wa habari  wakati wa mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Afya wa Serikali  ya wanafunzi IMTU, Vivian Mpangala.

1 comment:

alfred said...

serikali ishughulikie tatizo hilo ili chuo kiendelee kusaidia kuongeza idadi ya madaktari nchini.