Tangazo

October 3, 2011

CCM yang'ara IGUNGA


Jopo la wataalam wa CCM wakijumlisha matokeo usiku wa kuamkia leo, kutoka kwa mawakala wa CCM kutoka vituo mbalimbali baada ya uchaguzi mdogo jimbo la Igunga kumalizika. Hadi sasa matokeo yanaonyesha kwamba CCM inaongoza kwa zaidi ya kura 4000.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Katibu wa NEC Uchumi, Fedha, Mwigulu Nchemba na baadhi ya watu waliokuwa katika hoteli ya The Peak mjini Igunga wakishangilia usiku wakuamkia leo, baada ya kupata matokeo ya awali kutoka kwenye vituo kwamba CCM inaongoza.

Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) John Komba aking'ang'aniwa kwa furaha na watu waliopata matokeo ya awali kuwa CCM imeshinda.

Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma (katikati) akishangilia pamoja na wana-CCM wengine katika hoteli ya The Peak mjini Igunga baada ya kupata matokeo ya awali usiku wa kuamkia leo.

No comments: