Tangazo

October 3, 2011

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU YA WIZARA YA AFYA YAFUNGWA

Burudani ya Muziki kutoka kwa Mjomba Bendi katika kunogesha sherehe za kufungwa kwa maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru na Utoaji Huduma za Afya Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mafanikio yaliyofikiwa katika kutoa huduma ambazo hazikuwa zikipatikana hapa nchini kama vile Tiba ya Mfupa na Viungo, Upasuaji wa Moyo, Saratani na Tiba ya Magonjwa ya Figo pamoja na kusafisha Damu.
Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bw. Mohamed El Munir Safieldin akizungumza wakati wa kufungwa kwa maadhimisho hayo ambapo ameipongeza Tanzania kwa Mafanikio iliyofikia katika utoaji huduma za Afya katika Kipindi cha Miaka 50 iliyopita haswa katika kupunguza vifo vya watoto wadogo ambapo Tanzania kwa sasa imefanikiwa kupunguza vifo 110.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Lucy Nkya akitoa hotuba ya kufunga maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Afya na Serikali.
Mgeni rasmi Mhe. Lucy Nkya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mhe. Lucy Nkya akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Blandina Nyoni (kulia) wakizungumza na Muuguzi  kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Kitengo cha Uchunguzi wa Awali wa Saratani ya Kizazi, Maria Haule (kushoto).
Mmoja wa Wafanyakazi wa Chama cha Maalbino nchini akitoa maelekezo kwa  Mhe. Naibu Waziri juu ya Dawa wanazotumia walemavu wa ngozi kwa ajili ya kujikinga na madhara ya mionzi ya jua.
Mgeni rasmi na Ujumbe wake wakipata maelekezo kutoka kwa Sada Nabos Nachundu wa Nzasa W. Group wanaotengeneza bidhaa mbalimbali za lishe kwa kutumia unga wa zao la Mtama.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara na Serikali na wadau wa Sekta ya Afya nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Blandina Nyoni akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), Bw. Mohamed El Munir Safieldin. Picha na zainul Mzige wa MO Blog

No comments: