Tangazo

November 1, 2011

AKAUSHWA KAMA KUKU KWA IMANI ZA KISHIRIKINA IRINGA

UKATILI HUU.....!!!!!!  Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Laurance Nkwera (60) Mkazi wa Kijiji cha Ibani Ludewa katika Mkoa mpya wa Njombe, amekufa kwa kuchomwa moto na kuungua vibaya na watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina, huku nyumba yake ikiteketezwa vibaya kwa moto, na familia yake kunusulika kifo kwa nyumba hiyo kutobolewa.

Matukio kama haya yamekuwa yakitokea zaidi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa sasa hata mikoa ya Kusini imeanza kufanya vitendo hivi vya kikatili. Daily Mitikasi Blogu inalaani vitendo hivi kwani kuchukua sheria mkononi ni kosa la jinai na kuviomba vyombo vya dola kuwasaka wahusika ili kuwachukulia hatua kali za kisheria. Picha na Mdau Bazil Makungu

No comments: