![]() |
| Mmoja wa majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo, Abel Mwalukali akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kupigwa risasi kwenye mkono. |
![]() |
| Majeruhi wa risasi za polisi katika vurugu za Mwanjelwa leo hii akiwa kapigwa kichwani. Hadi sasa kuna majeruhi wanne wa risasi, wawili kichwani, mmoja kwenye paja na mwingine mkononi. |
| Msosi kitu gani bwana mbele ya uhai. |
| Mabaki ya ganda la risasi. |
| Mabomu ya machozi pia yalitumika. |
| Inapotokea patashika nguo kuchanika basi huwa hivi hata mzura huwa mzito kichwani.. |
| Maduka yote eneo la Mwanjelwa mpaka uyole yamefungwa. |
| Mmachinga akiwarushia jiwe polisi kwa kutumia manati yaani ni hatari tupu. |
| Moja ya gari lililobinuliwa na kuwekwa katikati ya barabara ya Mbeya-Tunduma. |
| Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana. |
| Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao.Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog |


No comments:
Post a Comment