Tangazo

December 27, 2011

TBL YAPANDA MICHE 4000 UWANJA WA SONGWE MBEYA

Wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya, wakiwa na miche ya miti kwa ajili ya kwenda kuipanda katika eneo la wazi katika Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizindua kampeni ya kupanda  miti katika eneo Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.

Mkazi wa Kijiji cha Ikumbi kilichopo jirani na Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Mbeya, akipanda moja kati ya miche 4000 iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupanda katika eneo la uwanja huo mwishoni mwa wiki.

Wakazi wa Kijiji cha Ikumbi kinachouzunguka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, wakipanda miti katika eneo la uwanja huo,mwishoni mwa wiki. Miche hiyo imetolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiwa ni kampeni ya kutunza mazingira.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akimwelekeza mtoto jinsi ya kupanda miti eneo la Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.

Mtoto akishiriki katika upandaji wa miti eneo la Uwanja mpya wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe jijini Mbeya mwishoni mwa wiki. TBL ilitoa miche 4000 na kuipanda kwenye eneo hilo ikiwa ni mikakati yake ya kuboresha mazingira.

No comments: