Tangazo

January 25, 2012

AIRTEL 'yazipiga Jeki' Vitabu Shule za Wilaya ya Siha

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Bw.Rashid Kitambulo akiishukuru kampuni ya Airtel kwa msaada mkubwa wa vitabu ilioutoa kwa shule nne za sekondari zailizopo wilayani hapo, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Oshara jana. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Oshara, Elieta Kaaya akifatiwa na Wawakilishi wa Airtel, Pascal Bikomagu na Jane Matinde na (kulia) ni Afisa Elimu Taaluma wa Sekondari Wilaya ya Siha,Bw. Mussa Shaban Ally.

                     ********************************************************************************
Airtel yatoa msaada wa vitabu kwa shule nne za sekondari wilaya ya Siha  mkoani  Kilimanjaro Chini ya mpango wake wa Airtel Shule Yetu ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo ambapo kila shule imepewa msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilling milio moja.   

Shule zilizonufaika na msaada huo ni za sekondari ya Oshara, Kilingi, Magadini na Namwai zote za wilayani humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa msaada huo na Mkurugenzi wa Mtendaji wa  Halmashauri ya  Wilaya ya Siha, Rashid Kitambulo ambaye alikabidhiwa vitabu hivyo na Afisa Uhusiano wa kampuni ya Airtel,  Jane Matinde.

Akiongea katika hafla hiyo,  Jane Matinde alisema " Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule hizi nne za sekondari wilayani Siha na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule hizi”.

“Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinua na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvu kazi ya kesho” Aliongeza Matinde.

Mgeni rasmi katika halfa hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Bw. Kitambulo alisema amefurahishwa kuona Airtel inajitoa katika kusaidia kuinua kiwango cha elimu nchini, moja kati mikakati ya elimu ya halmashauri hiyo iliyojiwekea ni kuhakikisha kwamba kila nyumba moja ya mkazi wa Siha anatoka 'graduate' na ili kufikia malengo yake kuna mahitaji makubwa ya vitabu vya kufindishia.

Aidha aliishukuru Airtel kwa kusaidia katika kutimiza malengo waliyojiwekea na kuwaasa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa wanafunzi na kufikia lengo halmshauri hiyo iliyojiwekea.

 Kwa upande wake Afisa Elimu Taaluma wa sekondari wilaya ya Siha Mussa Shaabani Ally aliishukuru Airtel kwa kuwawezesha vitendea kazi na kuongeza kuwa wilaya hiyo mpya bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu hivyo kuiomba kampuni hiyo kuendelea kuisaidia katika mambo mengine.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, wiki iliyopita Airtel ilitoa msaada wa kutoa kompyuta nne kwa shule ya sekondari Mlangarini iliyoko wilaya ya Arumeru mkoani Arusha na pia kuchangia katika sekta ya afya ambapo Airtel iligawa baskeli 10 kwa vituo vya afya wilayani Misungwi Mkoani Mwanza, hii ikiwa ni katika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

No comments: