Tangazo

January 13, 2012

KAMATI KUU YA CCM TAIFA YAMTEUA MOHAMED RAZA KUWA MGOMBEA WA NAFASI YA UWAKILISHI JIMBO LA UZINI

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kulia), akiendesha Kikako cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichokaa leo mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kuchagua mgombea atakayekiwakilisha Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi mdogo wa Uwakilishi katika Jimbo la Uzini, ambapo Kamati hiyo imemtangaza Mohamed Raza kuwa mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM. Kulia kwa Rais ni Makamu Mwenyekiti, Aman Abeid Karume, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed  Shein,  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Mjini Zanzibar jana, wakati akitangaza rasmi matokeo ya Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa.       
                       ***********************************************************

Na Sufianimafoto.blogspot.com, Zanzibar

Kamati Kuu ya CCM imemteua mwanachama wake, Mohammed Raza kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake.

Nape alisema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Aman Karume kufungua kampeni za CCM za kuwania jimbo hilo ambazo zitafanyika Januari 28, mwaka huu katika Uwanja wa mpira wa Ghana.

Alisema wakati kampeni zitafunguliwa na Dk. Karume, ufungaji kampeni hizo utafanywa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa mpira wa Tunduni.

Uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini unafanyika kufuatia kufariki dunia aliyekuwa mwakilishi wake kwa tiketi ya CCM, Mussa Hamis Silima aliyefariki kwa ajali ya gari, Septemba 23, mwaka jana.

Kuhusu minong’ono kwamba Raza ana utata katika uraia wake, Nape alisema Kamati Kuu imelitaza jambo hilo kwa makini lakini haikuweza kulipa uzito wa kumyima Raza nafasi ya kugombea kwa kuwa hakuna ushahidi wowote uliowasilishwa kuthibitisha hilo.

“Bado tunao muda wa kutosha, kama yupo mwenye ushahidi wa kutosha kuhusu hili anaweza kuleta ushahidi, ukiwa na uzito hatutaupuuza”, alisema Nape.

No comments: