Tangazo

January 13, 2012

Kitwana Manara afiwa na Mama yake Mzazi

Mama wa mwanasoka nyota wa zamani wa Tanzania, Kitwana Manara, Bi Mishi Mikessy, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya 95 amefariki duniani.

Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Kitwana alisema, Bi Mishi alifariki dunia juzi usiku baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Kitwana alisema Bi. Mishi anatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Waanglikana yaliyopo Buguruni-Malapa mjini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kitwana, marehemu B. Mishi ameacha watoto watano na wajuu kadhaa. Kitwana ni kaka wa wanasoka wengine nyota wa zamani nchini, Sunday Manara na Kassim Manara. Mwanasoka huyo mkongwe anaomba taarifa hizi ziwafikie ndugu na jamaa popote pale walipo.

Mungu ailaze roho ya marehemu Bi. Mishi mahala pema. Amin

No comments: