Tangazo

January 27, 2012

Matokeo ya Ubunge yatangazwa DRC

Rais Joseph Kabila

Matokeo ya uchaguzi ya Ubunge katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yametangazwa karibu katika maeneo mengi ya nchi

Chama tawala cha PPRD kimenyakuwa idadi kubwa ya viti 58 na muungano wa vyama vinavyoiunga serikali umenyakuwa idadi maradufu ya viti vilivyonyakuliwa na muungano wa upinzani unaomuunga mkono Etienne Tshisekedi.

Imeichukua tume huru ya uchaguzi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo takriban miezi miwili kukusanya matokeo ya kura hizo za ubunge ulofanyika wakati mmoja na uchaguzi wa urais tarehe ishirini na nan novemba mwaka jana

Mapema leo asubuhi maafisa wakuu wa tume hiyo wametangaza matokeo hayo ya viti 432 vya ubunge.

Mmoja kati ya kumi waliochaguliwa ni mwanamke, matokeo ya viti sitini na nane hayakutangazwa hasa katika mji mkuu kinshasa. Tume hiyo ya uchaguzi imesema majina ya washindi yatachapishwa jumatatu ijayo.
Etienne Tshisekedi.

Tume hiyo pia imewashauri wanaodhani waliibiwa kura zao kuwasilisha kesi mahakamani. Na bila shaka wengi wanatarajiwa kufanya hivyo kutokana na dosari nyingi zilizokumba uchaguzi huo na pia shughuli ya kuzihesabu kura.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na tume hiyo ,Chama tawala chake Rais Joseph Kabila cha PPRD kimepata viti hamsini na nane, chama cha upinzani cha Etienne Tshisekedi kimepata 34 ilhali washirika wa Rais Kabila wamepata ushindi maradufu ya viti hivyo vya upinzani.

Hata hivyo bado kuna hali ya kutoeleweka , wengi wakiwa wagombea wakibinafsi na vyama vingine vikiwa na viti kimoja au viwili tu. Karibu vyama mia moja vitawakilishwa katika bunge la nchi hiyo. Hii ina maanisha kwamba kutakuwa na haja ya kuungana kwa vyama kuweza kupitisha miswada ya sheria.

Rais wa tume ya uchaguzi , Daniel Ngoy Mulunda, amesema pia atawasilisha kesi katika mahakama kuu ya nchi hiyo kubatilisha matokeo ya majimbo saba ambayo yaliyokumbwa na vurugu za uchaguzi, na kuwafungulia mashtaka wagombeaji 14 akiwemo gavana wa mkoa mmoja kwa sababu ya kujihusisha na machafuko hayo.
Source: BBC Swahili

No comments: