Tangazo

January 26, 2012

ZAIDI YA BILIONI 128 KUKARABATI KM 172 ZA BARABARA ZA KOROGWE – MKUMBARA - SAME

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akiwekeana saini mkataba wa ukarabati wa  barabara ya Korogwe-  Mkumbara- Same pamoja na Mkandarasi kutoka kampuni ya  Strabag International GmbH ya Ujerumani  Meneja Biashara kwa Afrika Mashariki  Bw Karl Henz Schneder,   (kulia) jijini Dar es Salaam leo, Hafla hiyo pia imeshudiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt, John Magufuli (katikati alievaa miwani) akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti Kamati ya Miundombinu ambae pia na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, pamoja na watendaji wa ngazi za juu  wa Wizara ya Ujenzi na wadau wa sekta hiyo,Ukarabati huo wa km 172 utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 128 za kitanzania, ambapo kampuni hii itakarabati kipande kutoka  Korogwe - Mkumbara (76 km) na kugharimu zipatazo  shilingi bilioni 62.8  Hafla hiyo imefanyika Jan, 26,2012. ( Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) akibadilishana hati  na Mkandarasi ,   kutoka kampuni ya Strabag International GmbH ya  Ujerumani  ambae ni Meneja Biashara kwa Afika Mashariki Bw, Karl Henz Schneder baada ya kusaini mkataba. 

Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Barabara (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Mkandarasi kutoka  ya DOTT Services Ltd kutoka Uganda ambae ni Meneja  Mkuu Bw.G. Prudhvi Raj wakiwekeana saini mkataba wa ukarabati wa ujenzi wa barabara ya  Korogwe- Mkumbara- Same leo jijini Dar es Salaam, Mradi huo utagharimu  zaidi ya shilingi 12 bilioni, ambapo kampuni  hii itakarabati kapande  cha Mkumbara- Same (96 km) kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 65.1 za kitanzania.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) wakibadilishana hati na Bw.G. Prudhvi Raj baada ya kusaini mkataba.

No comments: