Tangazo

February 20, 2012

MABONDIA WALIOTEULIWA TIMU YA TAIFA WATAJWA

Makore Mashaga
Jumla ya mabondia 17 kutoka timu ya taifa ya ngumi wamechaguliwa kuendelea kubakia katika kikosi cha timu ya taifa katika mashindano ya mchujo yaliyo malizika tarehe 17.2.2012.

 Mabondia waliochaguliwa ni 49kg L-fly. John Christian na Said Pume.52kg fly.  Abdalah Kassimu na George Costantinee 56kg bantam, Emilian Patrick na Undule Langson 60kg i-weight.Denis Martine na Fabian Gaudence  64kg L-welter.Victor Njaiti na Hamisi Kitenge 69kg welter.Mohamed Mhibumbui 75kg middle.

Selemani Kidunda na Abdul Rashid 81kg l-heavy. Mhina Morris 91kg heavy.Haruna Swanga na Nuru Ibrahim 91-kg super heavy. Maxmillian Patrick.wote wanatakiwa kulipoti Ofisini katika shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini BFT tarehe 21.2.2012 ili wapewe taratibu za kuanza mazoezi .

Imetolewa na:
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)
Makore Mashaga
19/02/2012

No comments: