Tangazo

February 16, 2012

SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN LAZINDUA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UTAPIAMLO KWA WATOTO

Baadhi ya Wanafunzi hao wakiwa na Mh. Hilda Ngowi.

Mh. Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Iringa Lediana Ng'ong'o akizungumza na waandishi wa habari ambapo ametoa ushauri kwa  serikali kuwaajiri wataalam wa lishe kwa kila wilaya ili kufanikisha malengo ya Mkakati wa Kitaifa wa Lishe wa 2011/12 hadi 2015/16.

Mwanaharakati wa Haki za Watoto na Afya zao Bi. Hoyce Temu akizungumza na wanahabari kuhusiana na kampeni ya kupambana na utapiamlo kwa watoto, ambapo amesema tatizo hilo ni kubwa sana hapa nchini na kuishauri serikali ielimisha jamii umuhimu wa kula chakula bora na pia kutoa ufafanuzi kuwa chakula bora ni kipi.

Wanafunzi wakiandika mapendekezo yao kwenye Bango kubwa maalum la EVERYONE.

Dr. Ellen Otaru Okoedian akitoa mwongozo kwa wawakilishi wa mabaraza ya Wanafunzi kutoka wilaya za jiji la Dar es Salaam wakati Shirika la Save the Children lilipofanya uzinduzi wa taarifa ya Lishe  jijini Dar es Salaam Februari 15.12.

Wanafunzi wakiwa makundi kuandika mapendekezo wanayodhani yakifanyiwa kazi na Serikali yatasaidia kuhamaisha mpango wa kupambana na Utapiamlo kwa watoto.

Mh. Lediana N'gong'o na Bi. Hoyce Temu wakiainisha baadhi ya mambo muhimu yanayotakiwa kutekelezwa ili kufanikisha kampeni ya kupambana na utapiamlo hapa nchini.

Meneja Kampeni wa EVERYONE wa Tanzania Jasminka Milovanov (kushoto) akibadilishana mawazo na Bi. Hoyce Temu.

Mjadala wa Mapendekezo ukiendelea.

Makundi ya Wanafunzi hao katika picha ya pamoja na  Waheshimiwa Wabunge na waandaaji wa uzinduzi huo.

Hoyce Temu katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge.

No comments: