Tangazo

March 20, 2012

Afya ya Maalim Gurumo yaimarika

Msanii Mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Music, Muhidini Gurumo akiwa katika Hospital ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana, akipimwa mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospital hiyo, Suraiya Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita.Picha na habari kwa hisani ya burudan.blogspot.com
*******************
Na Mwandishi Wetu 
MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya  Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.

Akizungumza na Dar es Salaam jana, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super 'D' alisema Afya ya  Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina kujua kila kitu kinachomsumbua  katika mwili wake.

"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza akaruhusiwa hivi karibuni" alisema Super D.

Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo, kumuombea dua mwanamziki huyo ili apone upesi na kuwataka mashabiki wa bendi hiyo kuhudhuria maonesho yao ya wikiihii ni kama ifuatavyo;  Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani, Ijumaa watapiga katika viwanja vya Leaders Club, Jumamosi watakuwa katika viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni alisema Super D.

No comments: