Tangazo

March 20, 2012

TBL YASAIDIA SH. MIL 25 MRADI WA MAJI MKOLANI,GEITA

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamakale, Sizya Mulelemi Mashilungu akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25 Enock Kangasa, mkandarasi anayatekeleza mradi wa visima vya maji safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wananchi wa  kijiji cha Mkolani-1 Geita Mwanza, muda mfupi baada ya hundi hiyo kutolewa na kampuni ya Bia nchini (TBL),Wa pili kutoka kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa TBL Editha Mushi na kushoto wa kjwanza ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wilaya ya Geita Issa Msuya (mwenye shati la kijani).


Baadhi ya wananchi wa Nyamakale Mkolani -1 wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa TBL  Editha Mushi(hayupo pichani) kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 25 kusaidia mradi wa uchimbaji wa visima vya maji kijijini humo jana, katika wilaya ya Geita.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Geita, Daud Sweka kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo za kusaidia mradi wa visima vitatu  vya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa Kijiji cha Mkolani-1 wilayani humo hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mauzo wa TBL Geita, Issa Msuya.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (mwenye miwani) akipata maelezo  kutoka kwa mkandarasi, Enock Kangasa (mwenye shati jeupe la mikono mifupi ) ambaye anachimba visima vya maji  katika Kijiji cha Mkolani, Geita, kuhusu 'ring' zinazotumika katika ujenzi wa mradi wa visima vya maji uliofadhiliwa na  kampuni ya TBL  kwa sh. milioni 25. Hafla ya kukabidhi hundi ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Mkolani ambao pia watanufaika na mradi huo maji ya visima ambao TBL imefadhili shilingi milioni 25 kupitia mradi wake wa kusaidia jamii wa Hakuna maji Hakuna Uhai wakishuhudia makabiadhino ya hundi hiyo jana .

No comments: