Tangazo

March 19, 2012

Wanawake wa Kiislamu watakiwa kuwasomesha watoto wao elimu ya seqular: Mama Kikwete

 Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mke wa Rais Mama Salma Kiwete akisalimiana na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania  ( JUWAKITA) Mkoani Morogoro Machi 18.2012 alipohudhuria Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).   yalioandaliwa na jumiya hiyo ya JUWAKITA. (Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).

Wadau wa JUWAKITA kumsikiliza Mama Kikwete.

Wanafunzi wa madrasa wamsikiliza Mama JK.
********************************
Na Anna Nkinda – Maelezo,  aliyekuwa Morogoro

Wanawake wa Kiislamu nchini wametakiwa kuwahimiza watoto wao kwenda shule  na kujifunza elimu ya seqular  kwa kufanya hivyo wataweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika Dunia ya utandawazi  kwani masuala ya  kitaalamu yanahitaji wasomi ili kuweza kukabiliana na mazingira wanayoishi.

Wito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wanawake wa Jumuia ya Kiislamu (JUWAKITA) ya Mkoa wa Morogoro kwenye sherehe za  maulidi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mtume Muhammad (SAW) zilizofanyika katika chuo kikuu cha Kiislamu kilichopo mjini humo.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa kwa mazingira ya kawaida ya maisha  ya kila siku mtoto huwa na mama kwa muda mrefu zaidi kuliko baba katika kipindi chake cha utoto kwa msingi huo mwanamke ana majukumu makubwa ya kujenga familia iliyo bora na yenye maadili mazuri kwa kuwa muadilifu na kufanya mambo yanayompendeza Allah.

“Sisi tuliopo hapa tukiwa kama wazazi , walezi na viongozi wa dini inatupasa kuwaelimisha vijana wetu kumcha Mungu kwa kuwapa mafunzo ya kuijua Qur’an  na kufuata suna za mtume Muhamad  kwa kufanya hivyo tutajenga tabia njema miongoni mwao na hatimaye kuwa na taifa lenye maadili, utulivu na amani”, alisema mama Kikwete.

Aliendelea kusema kuwa ni jukumu la viongozi wa JUWAKITA pamoja na wanachama wote kuachana na mambo madogomadogo ambayo yatawarudisha nyuma kimaendeleo hivyo basi wapange mikakati ya kuiendeleza jumuia hiyo, kutekeleza majukumu waliyopewa kwa kushikamana na kuwa makini katika kutambua na kuainisha changamoto na hatimaye kuunda mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.

Akisoma risala  Mwenyekiti wa JUWAKITA wa Mkoa wa Morogoro,Zahra Kitima alisema kuwa katika jitihada za kuwapatia wanawake fursa zitakazowezesha kutatua matatizo yao  umoja huo  kwa kushirikiana na serikali, imedhamiria kuanzisha kituo cha mawasiliano, elimu,utamaduni  na habari ambapo itajumuisha  Maktaba  ya vitabu vya secular na dini, Computer laboratory,Ukumbi(matumizi mchanganyiko),kitengo cha nasaha kwa wasichana na eneo la vitega uchumi, ambacho kitawasaidia kutatua matatizo yao ya kidini, kielimu, kiuchumi na kijamii.


Kitima alisema, “Kitakapokamilika kituo hicho ambacho  kitakachogharimu zaidi ya Euro million saba na nusu kitaweza kuhudumia wanawake wapatao 180,000 kwa mwaka. Idadi kubwa ya watakaohudumiwa ni wanafunzi kutoka katika shule na taasisi za elimu mbali mbali hapa mkoani kwetu na mikoa ya jirani.

Halikadhalika, kituo pia kinatarajia kuendeshwa kwa kutumia rasilimali-watu, hasa wanawake, ambao watakuwa ni wanafunzi na wahitimu wa vyuo mbali mbali ambavyo Mungu ametujaalia kuwa navyo hapa mkoani Morogoro”.

Sehemu ya Sita ya Katiba ya BAKWATA, kifungu cha 99, kinaainisha kuanzishwa kwa Jumuia   ya Wanawake wa Kiislam Tanzania.Katika jitihada za kutekeleza maelekezo ya Katiba hiyo, mwaka 2011 Mufti wa Tanzania Sheikh Shaaban Simba, alimteua Mama Shamim Khan kuwa Mwenyekiti  Taifa wa JUWAKITA pia alimteua Hajat Mwatum Malale, ambaye  ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislam Morogoro(MUM)  kuwa  Katibu Mkuu.

No comments: