Tangazo

April 6, 2012

ASKARI WA KIKOSI CHA ANGA WATEMBELEA TBL DAR

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uhusiano na Kitengo cha Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo (kulia),  walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.

 Meneja wa Masuala ya Usalama mahali pa kazi wa TBL, Renatus Nyanda, akielezea kuhusu hatua mbalimbali za uzalishaji wa bia kiwandani hapo.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Kitengo cha Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo akisalimiana na maafisa hao.

Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, wakimsikiliza Mtaalamu wa Upishi wa bia, Richard Kagosi akiwaeleza jinsi bia inavyopikwa kwa kutumia kompyuta   walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL.

 Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Anga, wakiingia kutembelea kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea jinsi bia zinavyozalishwa pamoja na kujifunza masuala ya Usalama mahali pa kazi, afya ya wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Your Solutions Tanzania Limited, Damian George akionesha kifaa cha kisasa cha kuzimia majanga ya mato yanapotokea.

Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha Anga, akielekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni yaYour Solution Tanzania Limited, Damian George, jinsi ya kukitumia kifaa cha kisasa cha kuzimia moto kiitwacho DSPA, walipotembelea kiwanda cha bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, kujifunza masuala ya usalama kazini, afya za wafanyakazi na utunzaji wa mazingira.

Askari wakisikiliza kwa makini walipokuwa wakipata maelezo ya jinsi ya kukitumia kifaa hicho cha kuzimia moto.

No comments: