Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, habari zinasema mwili wa mwigizaji huyo umepelekwa katika hospitali ya taifa ya Muhibili ili kuhifadhiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, amethibitisha juu ya kifo cha mwigizaji huyo na kuongeza kwamba sababu za kifo chake bado zinafanyiwa uchunguzi lakini taarifa za mwazo ambazo polisi wamezipata zinasema Kanumba alikuwa na mpenzi wake chumbani na kulitokea kutokuelewana kati yao na kusababisha kukatokea kwa ugomvi ulipelekea kifo chake.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA AMEN |
No comments:
Post a Comment