Tangazo

April 25, 2012

Safari Lager yatangaza kukamilika kwa Mafunzo ya Wajasiriamali wa “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu kukamilika kwa mafunzo ya wajasiliamali wa “Wezeshwa na Safari Lager”  Dar es Salaam jana.Kulia ni Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiliamali kutoka kwenye taasisi ya TAPBDS, Joseph Migunda.

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akiwaonyesha waandishi wa habari namna ya kuipata fomu ya kuomba ruzuku ya “Wezeshwa na Safari Lager” kwa awamu ya pili wakati wa kutangaza kukamilika kwa mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiliamali kutoka kwenye taasisi ya TAPBDS, Joseph Migunda.
*********************
 Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi kukamilika kwa mafunzo ya wajasiriamali waliopatikana katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema mafunzo kwa wajasiriamali wa “Wezeshwa na Safari Lager” yalikamilika rasmi mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya.

Aliwapongeza wajasiriamali wote waliofaulu na kupatiwa mafunzo haya yanayolenga kuwawezeshwa kupanua na kukuza biashara zao. Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili.

Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea

Shelukindo alisema “Ni jambo jema kwamba wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano

Bwana Shelukindo aliwataja wajasiriamali waliomaliza mafunzo na watapatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali walifaulu ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Martin Richard Tupilike, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi.

Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.

Bwana Oscar Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali waliofaulu katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja.

Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.

Bwana Shelukindo aliendelea kusema “Safari Lager tunayofuraha kubwa kuwasaidia wajasiriamali hawa, tunawapa pongezi kwa uvumilivu wao na jitihada kubwa waliyo nayo. Tutawakabidhi vitendeakazi vyao katika hafla maalumu kuanzia wiki mbili zijazo”.

Akielezea mafunzo yalivyoendeshwa Bw. Joseph Migunda wa taasisi ya TAPBDS alisema wajasiriamali katika mikoa yote wameonyesha uelewa kwa kiwango cha juu na wote walifaulu mtihani wa kuhitimisha mafunzo hayo. Alisema “Tuna imani wajasiriamali watatumia elimu na ruzuku wanayopatiwa ili kupiga hatua zaidi kufikia ndoto zao”.

Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano hili, aliendelea “Shukrani nyingi sana ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lager baadae mwaka huu.

No comments: