Tangazo

April 25, 2012

Mbunge wa Viti Maalumu Katavi (CCM), Prudenciana Kikwembe athibitisha Kuporwa Fedha

Mh. Prudenciana Kikwembe
Katika taarifa yake aliyoisambaza katika Vyombo vya Habari leo Mheshimiwa Prudenciana Kikwembe ni kweli kuhusu tukio la kuporwa fedha na kadi za benki kama ilivyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma.
 
Aidha amesema ni kweli tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 2.30 (saa mbili na nusu) usiku katika baa ya Lady May Pub, iliyoko barabara ya Iringa.
 
Mheshimiwa kikwembe anasema alilifika mahali hapo kwa ajili ya kupata chakula pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu zilizoko mkoano Dodoma wanaotoka Rukwa na Katavi kuhuasiana na mambo mbalimbali.
 
Miongoni mwa mambo hayo ni hatma ya  Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye anatoka katika mkoa wa Katavi (zamani Rukwa kabla ya kugawanywa na kuwa mikoa mwili ya Rukwa na katavi).

Kwani wanafunzi haowalikuwa na shauku ya kujua hatima hiyo kutokana na mambo yalivyokuwa yamejitokeza ndani ya Bunge.
 
" Nimependa kuweka hili ili kuiwezesha jamii kufahamu yaliyojiri na pia kueleza ukweli kwani wapo baadhi ya watu ambao wameanza kutafsiri tukio hili kwa namna tofauti kwa sababu wanazozijua" sehemu ya taarifa inasema.
 
Sambamba na hilo, wanafunzi hao walikutanae ili kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika mikoa yao ya Rukwa na Katavi pamoja na suala la ajira na mambo yanayowahusu kuhusiana na masomo.  
 

No comments: