Tangazo

April 25, 2012

KESI YA CHARLES TAYLOR KUTOLEWA HUKUMU APRILI 26

Charles Taylor
Na Hirondelle, Freetown

 Ikiwa umepita zaidi ya mwaka mmoja tangu kesi dhidi ya kiongozi wa zamani wa Liberia, Charles Taylor kuhitimisha hoja za mwisho mbele ya Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCSL), sasa mahakama hiyo itatoa hukumu Alhamisi, Aprili 26.

Taylor anashitakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, yaliodaiwa kufanywa kati ya Novemba 30 1996 na Januari 18, 2002.Kwa mujibu wa mwendesha mashitaka, Taylor alifadhili, kutoa mafunzo na kuwapatia silaha waasi wa RUF, kwa lengo la kuiba dhahabu kutoka nchini Sierrea Leone.

Kesi yake ilianza kusikikilizwa Juni 2007. Mwendesha mashitaka aliita mashahidi 94, wakiwemo 32 waliokuwa marafiki wa karibu wa Taylor ambao walitoa ushahidi dhidi ya yake.

Waathiriwa wengi wa uhalifu wa RUF, walitoa ushahidi dhidi ya Taylor, akiwemo Joseph Marzah, maarufa kwa jina la Zig Zag, muuaji ambaye anadaiwa alikuwa anatekeleza amri za Taylor juu ya ‘’namna ya kupika kofia ngumu ya chuma’’ au jinsi ya kuua ‘’watoto.’’

Vita vya wenye kwa wenyewe Sierra Leone, viliacha watu 150,000 wakiwa wamekufa na wengine kwa maelfu wakiwa wamekatwa mikono, baada ya waasi kuwataka kuchagua kati ya ‘’mikono mifupi’’ au ‘’mikono mirefu.’’

Mashahidi wengine walisema kwamba Taylor alikula njama za kukubaliana na waasi wa RUF kufanya biashara ya dhahabu kwa ajili ya kupata silaha.Ibrahim Bah na Benjamin Yeaten, ambao ndiyo wanaodaiwa kupanga makubaliano hayo na Taylor hawajashitakiwa kamwe na ICC.

Upande wa mwendesha mashitaka pia ulitoa ushahidi kwamba mshitakiwa  katika kipindi cha miaka mitatu alipewa dola za Kimarekani milioni 14, ambazo zilitumbukizwa katika akaunti yake binafsi katika Benki ya Liberia.

Taylor aliiambia mahakama kwamba akaunti hiyo ya siri iliwekwa ili kukwepa vikwazo vya silaha vilivyowekwa dhidi ya Liberia na jumuiya ya kimataifa.

Timu ya utetezi kwa upande wake iliita mashahidi 21, akiwemo Taylor mwenyewe, ambaye ushahidi wake ulichukua miezi mitano. Alikuwa anajaribu kuwashawishi majaji kwamba yeye siyo ‘’mbabe wa vita’’ bali ni’’mtu wa amani,’’ na ‘’mwana mapinduzi’’ zaidi kuliko ‘’gaidi.’’

Taylor anadai pia kwamba kesi yote hiyo ni ‘’njama’’ zilizoandaliwa na Marekani baada ya kuukataa mpango wa kanda wa Halliburton, kampuni ya mafuta ya Marekani.

Taylor aliandaliwa mashitaka Juni 2003 lakini hati ya kukamatwa kwake ilibakia kuwa siri hadi alipokubali kuachia madaraka Agosti 2003, bada ya kupewa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchini Nigeria. Machi 2006, alitiwa mbaroni nchini Nigeria na kisha kusafirishwa hadi katika mahakama ya SCSL.

Serikali ya Uholanzi ilikubali kupokea kesi hiyo kusikiliziwa nchini mwake kufuatia ombi la Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye alikuwa anahofia kuzuka kwa ghasia iwapo kesi hiyo ingesikilizwa Sierra Leone.

Hukumu hiyo itakayotolewa na SCSL itakuwa ya kwanza kutolewa na mahakama ya kimataifa dhidi ya aliyekuwa mkuu wa nchi. Kama Taylor atatiwa hatiani atatumikia adhabu yake nchini Uingereza.

No comments: