Tangazo

April 6, 2012

VODACOM YATOA MIKOPO KWA AKINAMAMA WA MKOA WA PWANI

Meneja wa mradi wa MWEI unaondeshwa na Vodacom Tanzania, Mwamvua Mlangwa ,akimkabidhi F edha  Radhia Abdalah, ambazo ni mkopo usio na riba inayotolewa na kampuni hiyo na kurudishwa kwa njia ya m-pesa,zaidi ya shilingi Milioni 30 zimetolewa kwa vikundi vya kinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga kilichopo Mlandizi mkoani  Pwani,Jumla ya kinamama 425 wamenufaika na mkopo huo.

Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule akifafanua jambo kwa wakina mama wajasiliamali wa Mlandizi Mkoani Pwani ,kuhusiana na matumizi ya mikopo waliyopewa na Vodacom Tanzania kupitia mradi wa MWEI,Vodacom kupitia mradi huo umewanufaisha  jumla ya wanawake 425 kwa kuwapa mikopo isiyo na riba wa zaidi ya shilingi Milioni 30 Mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimkabidhi fedha Mwanaidi Said ambae ni mmoja wa akinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga cha Mlandizi Mkoani Pwani ,Fedha hizo zilitolewa na Vodacom Tanzania  kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiliamali na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya m-pesa bila riba. Jumla ya kinamama 425 walinufaika na mkopo huo wenye thamani ya zaidi ya shilingimilioni 30. Katikati ni Meneja mradi huo Mwamvua Mlangwa. 

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akimkabidhi fedha Khadija Khalifan ambae ni mmoja wa akinamama wajasiliamali wa kikundi cha Kilangalanga cha Mlandizi Mkoani pwani ,Fedha hizo zilitolewa na Vodacom Tanzania  kupitia mradi wake wa MWEI kwa ajili ya kusaidia wakinamama wajasiriamali na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya m-pesa bila riba. Jumla ya kinamama 425 walinufaika na mkopo huo wenye thamani zaidi ya shilingimilioni 30. Katikati ni Meneja mradi huo Mwamvua Mlangwa na Kuliani Diwani wa kata ya Janga Mlandizi Fedilia Simba.

No comments: