Tangazo

March 10, 2014

UPDATES: MAMA ALIYETOROKA NA MTOTO ALIYEUNGUA NA MOTO APATIKANA NJOMBE

Hatimaye Mama aliyetoroka na mtoto aliyeungua moto apatikana kupiga  simu katika Chombo cha Mbeya yetu Blog  kuwa yupo Njombe kwa baba mzazi wa mtoto huyo nakuomba radhi kuwa aliondoka bila kuaga kesho saa nane mchana atakuwa amerudi na mtoto huyo 

Mama huyo amejitokeza baada ya mtandao wa Mbeya yetu kuandika mapema leo kwamba alikuwa ametoweka bila Taarifa zozote, Akiongea na Mbeya yetu amedai kwamba yeye aliondoka ili akashauriane na wazazi wa Mtoto huyo ili waone ni jinsi gani watamsaidia lakini alipo hojiwa amejikanyaga kanyaga na kuongea bila kuwa na uhakika na kile anacho zungumza.

Hata hivyo hapo kesho atafanyiwa mahojiano ya kina na kuona ukweli ukowapi kwa kuwa anatia mashaka na maelezo yake, Tunaendelea kusisitiza kuwa Kama kuna Mtu anahitaji kumchangia mtoto huyo asifanye hivyo kwa kuwa mama huyo kasha onesha wasiwasi na kuondoa imani watu.
Habari zaidi zitakuja

Huyu ndiye Mama Mkubwa wa Mtoto Adolotea Nyavike bi. Salome Kiegu(35) ambaye alitoweka  na mtoto huyo kusiko julikana huku wasamalia wema wakitaka kutoa misaada.

No comments: