Tangazo

May 31, 2012

DROO YA TANO YA PROMOSHENI YA VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO NA SBL, YANGURUMA TENA, MWANZA WAENDELEA KUVUNA ZAWADI

Meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager, Bw. Allan Chonjo akizungumza wakati wa kutangaza washindi wa Jenereta na Bajaj katika bahati nasibu ya promosheni ya Vumbua Hazina chini ya Kizibo iliyofanyika kwenye ofisi za Kampuni hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam. Katikati ni Tumainiel Malisa kutoka PWC na (kulia) ni Abdallah Hemed kutoka Bodi ya Mchezo ya Kubahatisha.
*********************

Zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi waliojitokeza kushiriki na kushinda zawadi zinazotolewa katika promosheni ya kipekee ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti limeendelea wiki iliyopita katika mikoa ya Iringa na  Mwanza ambapo mshindi wa jenereta na yule wa bajaj walikabidhiwa zawadi zao katika sherehe zilizohudhuriwa na umati mkubwa wa watu na kushuhudia SBL ikikabidhi zawadi hizo na kuamsha hamasa kubwa kwa wapenzi na watumiaji wa biadhaa za SBL.

Asubuhi ya leo droo ya tano ya promosheni hiyo ‘VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO’ imechezeshwa katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti zilizopo maeneo ya Oysterbay jijini na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari, wasimamizi kutoka Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania, wadau kutoka ndani na nje ya kampuni hiyo, wakiwemo kampuni ya kuendesha Bahati Nasibu ya PUSH MOBILE na wahakiki na wakaguzi kutoka PWC-Price Water House Coopers.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa kuchezeshwa kwa droo ya tano ya promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo bw. Ephraim Mafuru, amesema “Tumeshakabidhi jereta nne kwa washindi mbalimbali na zawadi ya pikipiki, bajaj mbili na gari moja aina ya FORD FIGO ambapo zawadi zote zimeshakabidhiwa kwa washindi wetu .  Hivi karibuni tutasafiri  kwenda Mafinga Mkoani Iringa kukabidhi Bajaj”.

“Naendelea kuwashauri jamii na watanzania kwa ujumla kwamba promosheni hii ni kwa ajili ya kila mtanzania mwenye vigezo vya kushiriki kwa hiyo wajitokeze k kwa wingi kushiriki ili kujaribu bahati kama wenzetu ambao wamejaribu na kupata zawadi kubwa ambazo hawakutarajia katika maisha yao.” Alisema  Mafuru.

Aliongeza kuwa zawadi zinazoshindaniwa gharama yake ni jumla fedha za kitanzania milioni 780 ikiwemo pesa taslimu ambazo mshindi anapata papo hapo kupitia matandao wa simu za mikononi M- pesa. Ikumbukwe kuwa zawadi hizi zinapelekwa hadi pale mshindi wetu alipo bila yeye kuchangia chochote walakugharamia chochote ikiwemo usafiri.

Katika droo hii ya tano mshindi ni Isaya Charles kutoka Igoma mkoani Mwanza ambaye amejishindia Jenereta, wakati mshindi mwingine Mariam Karumba mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Saint Agustin pia anatoka mkoani Mwanza amejishindia Bajaj

Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bidhaa yake bora kabisa ya Serengeti Premium Lager, Tusker Lager and Pilsner inaendesha promosheni hii kwa wiki 16 ikiwa na lengo la kuinua na kuboresha maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla.

No comments: