Tangazo

May 31, 2012

Safari Lager yatangaza Zawadi kwa Wajasiriamali Washindi wa “WEZESHWA NA SAFARI LAGER"

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika programu ya ruzuku ya“Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam leo.Vifaa hivyo vitakabidhiwa mwishoni mwa wiki katika viwanja vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya.
**************Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa  kwa wajasiliamali  ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali walioshinda katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali.

Shelukindo alisema, “Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. 

Aliendelea, “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09 June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye viwanja vya leaders Club.”

Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hao, Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. 

Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. 

Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea.

Akionyesha baadhi ya ruzuku zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda “wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano" alisema.

Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. 

Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi na Damas Daniel Msoka.

Wengine ni pamoja na Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi.

Aidha aliwataja washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.

 Kituo cha Mwanza ni pamoja na Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. 

Katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwaluaja na Tatu Ngemela.

No comments: