Tangazo

May 2, 2012

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGUA CHUO KIPYA CHA VETA MKOANI MANYARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi wa Korea Kusini, Young Hoon Kim, kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakati wa hafla ya ufunguzi wa chuo hicho iliyofanyika Aprili 30, 2012, mkoani Manyara. Picha na  Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano:- wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo kipya cha VETA, baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichojengwa Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara. Hafla ya ufunguzi wa Chuo hicho ilifanyika Aprili 30, 2012, mkoani Manyara. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mwalimu wa ufundi wa Magari wa Chuo kipya cha VETA cha Mkoani Manyara, Treekta dogo linalotumika kulimia na kupandia Mbegu za mazao, wakati aliokuwa akitembelea na kukagua majengo mapya ya Karakana ya chuo hicho baada ya kukifungua rasmi  Aprili 30, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na viongozi wa Chuo cha Veta na viongozi wa Serikali baada ya ufunguzi rasmi wa chuo hicho uliofanyika  Aprili 30, 2012 mkoani Manyara. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: