Tangazo

May 2, 2012

Wake za Viongozi Wakuu wa Serikali watembelea kambi ya Taifa Queens na kuhani msiba kwa Mzee Sumaye

Wake wa Viongozi Wakuu wa Serikali ambao ni wananchama wa New Millenium Group wakishuhudia mazoezi ya timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi iliyopo Kibaha, Mei Mosi 2012.  Kutoka kushoto ni Regina Lowassa, Zakia Bilal, Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Bayi, Tunu Pinda, Anna Mkapa, Asha Bilal na Khadija Mwinyi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akimkabidhi Mwenyekiti wa Chama za Netiboli Tanzania (CHANETA), Anna Bayi moja kati ya katoni 40 za maji ya kunywa wakati wake wa viongozi  walipotembelea kambi ya timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens kwenye shule ya sekondari ya Filbert Bayi, Kibaha Mai 1, 2012.  Kuklia ni Mke wa Mkamu wa Rais, Mama Zakia Bilal  na watatu kulia pia ni  Mke  wa Makamu wa Rais, Mama Asha  Bilal kushoto ni Mama Hasna Kawawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipa Pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Esther Sumaye ambaye hivi karibu alifiwa na baba yake mzazi Mzee Natai wakati alipoongoza ujumbe wa wake wa viongozi ambao ni wananchama wa kikundi za New Millenium Group kwenda kuhani msiba huo, nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu (Frederick Sumaye (watatu kulia) Kibaha Mei Mosi, 2012. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: