Tangazo

May 14, 2012

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AZINDUA BLOG NA TOVUTI RASMI YA CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jaklaya Kikwete akizindua Blogu na Tovuti  Rasmi vyote vya Chama, hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Wanaomwelekeza ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Suleyman Mwenda ambaye ni Mkuu wa Masuala ya Teknolojia na Mawsiliano, Idara ya Mawasiliano na Umma Makao Makuu ya CCM. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) John Chiligati na Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) Vuai Ali Vuai. Tovuti ya CCM ni www.ccm.or.tz

Nape akitoa maelezo kuhusu Tovuti na Blogu hizo zinavyoendeshwa na faida zake kwa CCM.

Rais Kikwete akiwa na mwenyeji wake katika uzinduzi huo Nape Nnauye wakati akiwasili.

Nape akimshauri jambo Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Amani Abeid Karume.

Nape akitoa hotuba fupi kuhusu Tovuti na Blog.

Katibu wa CCM Wilson Mukama wakati alipomkaribisha Rais Kikwete kuzindua Blogu na Tovuti (Website Rasmi ) ya Chama.



Ikafuatia burudani ya hali ya juu iliyoporomoshwa na bendi ya Super Melody ya CCM. huku Nape akionyesha umahiri wake wa kucharaza gita na bendi hiyo.

 Wakati anaondoka Mjumbe wa NEC Mzee Mtandika akionyesha umahiri mbele yake wa kusakata muziki wa enzi hizo.

No comments: