Wananchi na polisi wakisaidiana kuinasua miili ya watu watatu walio kufa katika ajali. |
Ubongo ukiwa umetapakaa katika eneo la ajali. |
Hivi ndivyo Fusu lilivyokuwa baada ya ajali. |
Mwili wa dereva Taxi ukiwa umenasa.
|
Ajali mbaya imetokea mjini Iringa asubuhi ya leo na kusababisha watu watatu kufa papo hapo huku abiria waliokuwemo katika lori aina ya Fuso wakinusurika katika ajali hiyo.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa Taxi hiyo yenye namba za usajili T620 ANE ilikuwa ikitokea Ndiuka ikiwapeleka wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara katika eneo la Tanangozi ambako ujenzi wa barabara Kuu ya Iringa -Mbeya unaendelea.
Hata hivyo kabla ya kufika katika eneo hilo la kituo cha Mafuta cha Esso, dereva wa Taxi hiyo ambaye alikuwa akitaka kulipita gari jingine lililokuwa mbele yake alishindwa kulipita gari hilo baada ya kukutana uso kwa uso la Fuso yenye namba za usajili T897 AQS ambalo lilikuwa limeshehena magunia ya mpunga .
Hivyo kutokana na mwendo kasi ambao Fuso hilo lilikuwa likienda na mwendo kasi wa Taxi hiyo uwezekano wa kukwepana ulishindikana na hivyo kupelekea Fuso hilo kuigonga Taxi hilo na kuipitia kwa juu na kupelekea vifo vya abiria wawili na dereva wa Taxi hiyo.
Jitihada za kuzitoa maiti hizo zinaendelea hadi sasa japo eneo la tukio likiwa limetapakaa ubongo wa maiti hizo za ajali na wasamaria wema wakiendelea kufanya kazi hiyo ya kuzitoa maiti bila ya kutumia kinga yeyote na hivyo idadi kubwa ya wasamaria wema hao waqmeonekana wakiwa wametapakaa damu.
Habari na Picha kwa Hisani ya www.francisgodwin.blogspot.com
No comments:
Post a Comment