Tangazo

May 3, 2012

WAZIRI MAGUFULI AKAGUA MIRADI YA DART NA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-TEGETA JIJINI DAR

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli akitoa ufafanuzi wa mradi wa mabasi yaendao mwendo kasi (DART) kwa waandishi wa habari alipotembelea na kuangalia maendeleo ya  mradi huo jijini Dar es Salaam Mei 2.2012 . Mradi huo utagharimu shilingi bilioni 288/- ambazo zitajumlisha kwa pamoja na ujenzi wa vituo vya mabasi. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

Waziri wa Ujenzi, Dk, John Magufuli akikagua upanuzi wa Barabara ya Mwenge - Tegeta jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa  wa DSM, Mwantumu Mahiza.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wa DART  Mei 2,  kwa Waziri wa Uchukuzi  Dk. John Magufuli (kushoto). Mradi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano wa  magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jijini.

Mkurugenzi Mtendaji wa mradi wa mabasi yaendayo mwendo kasi jijini Dar es Salaam (DART),  Cosmas Takule akitoa maelezo ya mradi huo kwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (hayupo pichani).

No comments: