Tangazo

June 28, 2012

ICTR YAENDELEA KUHAHA KUTAFUTA NCHI ZA KUWAPOKEA WALIOACHIWA HURU

Na Hirondelle, Arusha

 Rais na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wanaendelea kuhaha kutafuta nchi za kuwapokea washitakiwa walioachiwa huru na mahakama hiyo.

Rais wa ICTR, Jaji Vagn Joensen aliliambia Shirika la Habari la Hirondelle kwamba ‘’Msajili na mimi tutazidisha juhudi zetu za kidiplomasia kutafuta nchi zitakazofaa kuwapokea waliochiwa huru.’’ ‘’Katika hutuba yangu niliyoitoa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Juni 8, mwaka huu, nililiomba Baraza la Usalama kutoa wito kwa nchi zote kushirikiana nasi katika kulipatia ufumbuzi tatizo hili.’’alisema.

ICTR inatarajiwa Jumatatu ijayo kukabidhi baadhi ya majukumu yake kwa taasisi mpya itakayorithi kazi zinazobakia za mahakama hiyo ijulikanayokamaInternational Residual Mechanism (IRM).

Tatizo la kupata nchi za kuwapokea washitakiwa wanaoachiwa huru na ICTR bado linaumiza vichwa vya wakuu wa ICTR licha ya wito mbalimbali uliokuwa unatolewa na mahakama hiyo siku za nyuma.

‘’Ugumu utabaki kuwa uleule, yaani kukosa utayari wa nchi kuwapokea wanaoachiwa huru katika ardhi yao, kwa sababu wanazozifahamu wenyewe,’’ Msemaji wa ICTR, Roland Amoussouga aliiambia Hirondelle, Novemba mwaka jana.

Mahakama ya Rufaa ya ICTR imeshathibitisha kuachiwa huru kwa watu watano lakini bado hawajapata nchi za kuwapokea.Watu hao ni pamoja na jenerali mmoja wa jeshi, mawaziri watatu na shemeji wa Rais wa zamani waRwanda, marehemu Juvenal Habyarimana.

Wote hao wanataka kuungana na familia zao zinazoishi Ulaya, wengi wao wakiwa wameshapata urai wa nchi hizo.

No comments: