Tangazo

June 25, 2012

NUKUU YA LEO

"Tunavyoandika kuhusu au kusimulia kuhusu wachezaji wa Ulaya inakuwa kama ni majirani zetu. Ukisikiliza utadhani mtu anachambua sana soka la Ulaya kumbe anatafsiri stori iliyoandikwa na mwandishi wa Ulaya. Ukimwambia mtu huyo huyo achambue mechi ya Simba na Yanga, utagundua kuwa kumbe hajui uchunguzi wowote. Tufikie kiwango cha uandishi wa wenzetu wa barani Ulaya ambao wanafanya utafiti wa nguvu kabla ya kuandika habari au kwenda live studio. Thom Mhalmbo alisema anatumia masaa mawili kufanya utafiti kwa kupiga simu kwa ma-source mbalimbali na kupitia internet. Wenzetu wanatumia nusu saa kutafsiri stori za walio juu halafu wanatumia neno "nafikiri" kuonyesha kuwa wanatumia akili sana!!" Nukuu ya Angetile Osiah (pichani), Katibu Mkuu wa TFF na Mwandishi wa Habari Mwandamizi nchini, kutoka katika ukurasa wake wa Facebook

No comments: